Facebook

Sunday 22 June 2014

Wafahamu mastaa wa Bongo waliotoka familia bora zenye uwezo

Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua
basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni
wale watoto waliozaliwa kwenye familia
zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora. Mara
nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha
duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo
sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa
pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia
A’level , Hawa wengine walikua wapo shule
wakisoma na kuishi vizuri.
Hawa ndo baadhi ya watoto wakishua
ambao kwasasa ni celebrities…

Vanessa Mdee

Vanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee au
Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988.
Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy
Mdee (kwasasa ni marehemu )ambaye alikua ni
mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia.
Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri
nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia
miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.

Nisher

Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii
GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya
Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher
amekulia katika maisha mazuri na hadi ni
wakishua bado. Baba yake aliweza kumsaidia
Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya
milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji
alichonacho.

Jokate Mwengelo

Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay
kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya
kazi serikalini. Kumbuka Jokate alizaliwa
washington DC nchini Marekani ambapo wazazi
wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza
high school katika shule ya Loyola ndipo
alipogombania Miss Tanzania mwaka 2006 na
kushika nafasi ya 2.

Lucci

Jina lake halisi anaitwa Luciano Tsere au
unaweza kumuita Lucci ambaye ni producer
maarufu nchini. lucci amezaliwa tarehe 30
September mwaka 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni
mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa
mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao. Lucci
naye kama jokate amekulia Obey kwenye familia
bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa
Tanzania.

Wema Sepetu

Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye
Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho
katika familia ya wasichana wanne wa Balozi
Isaack Sepetu Ibrahimu (marehemu).Wema
sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika
hospitali ya ST. Andrew’s jijini Dar es Salaam na
ni mtoto wa mwisho kuzaliwa huku
akisoma elimu yake ya primary na sekondari
katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL
iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda
Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za
kimataifa katka chuo cha Limkokwing University

0 comments:

Post a Comment