Barcelona imemsajili kipa mwingine baada ya kumnasa Marc-Andre ter Stegen.Golikipa huyo anaitwa Claudio Bravo alikuwa anakipiga katika klabu ya Real Sociedad,na anadakia timu ya taifa ya Chile na yuko na timu hiyo katika michuano ya kombe la dunia huko Brazil hivi sasa.Claudio Bravo mwenye miaka 31 amesaini mkataba wa miaka 4.Anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Barcelona baada ya golikipa mwingine Marc-Andre ter Stegen na kiungo kutoka Sevilla na timu ya taifa ya Croatia Ivan Rakitic.
Imeandaliwa na .....
Katemi Methsela
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment