Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika.
Kenyatta amempiku Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma.Rais wa Afrika Kusini anayesifika kwa kashfa mbali mbali, Jacob Zuma ana wafuasi 325,896 akishikilia nafasi ya tatu.
Hata hivyo swali ni je maerais hawa hutumia vipi Twitter? Je wao huwa na mazungumzo ya moja kwa moja na wafuasi wao?
Waziri mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi '@AmamaMbabazi,' ndiye kiongozi mwenye kuwasiliana zaidi na wafuasi wake duniani kwenye Twitter huku akiwajibu maswali yao kwake.
Waziri mkuu mpya wa India, Narendra Modi ana wafuasi milioni 4,967,847 , na anaelekea kushinda Ikulu ya white House ambayo ina wafuasi milioni 4,976,734 katika nafasi ya tano.
Zaidi ya asilimia 83 ya mataifa yote duniani yana uwakilishi katika Twitter, na asilimia 68 ya viongozi wana akaunti za twitter kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Burson-Marsteller, nchini Marekani.
Viongozi wanaofuatwa sana kwenye Tiwtter ni pamoja na Barack Obama (@BarackObama) akiwa na wafuasi milioni 43, Papa Francis (@Pontifex) ana wafuasi milioni 14 akifuatiwa na Rais wa Indonesia Susilo Bambang Yudhoyono (@SBYudhoyono) akiwa na wafuasi milioni tano.
Kati ya serikali 643 zenye akaunti za Twitter ambazo zilitathminiwa katika nchi 161, ni mataifa 32 pekee hasa yaliyo Afrika na Asia ya Pacific ambayo hayana shughuli nyingi kwenye Twitter.
Utafiti huo pia ulifichua kuwa mawaziri wa mataifa ya kigeni hutumia sana Twitter kutafuta ushirikiano wa kidiplomasia.
0 comments:
Post a Comment