Rio Ferdinand amekubali kujiunga na QPR baada ya kukaa Manchester United kwa miaka 12 (Daily Mail),
Angel Di Maria wa Real Madrid anasakwa
 na Manchester United na Arsenal, na amekiri kuwa hana uhakika wa kuwepo
 Madrid msimu ujao (Daily Express), 
Meneja mpya wa Southampton amewatikisa Man United kwa kuongeza bei ya 
beki Luke Shaw kwa pauni milioni 10 zaidi, hadi kufikia pauni milioni 40
 (Daily Mail), 
Baba Mkwe wa Luis Suarez amesema huu ni wakati muafaka 
kwa mchezaji huyo kuhamia Real Madrid au Barcelona kwa sababu hana 
"chochote cha kuthibitisha England" (La Sexta), 
Chelsea wamesema 
hawatomruhusu Romelu Lukaku kwenda kwa mkopo timu yoyote msimu ujao 
(Daily Express), 
Tottenham, Hull City na Manchester United wanafikiria 
kumwania beki wa Espanyol Hector Moreno (Marca),
 Mshambuliaji wa Swansea
 Michu yuko njiani kuhamia West Ham kwa pauni milioni 6 (Sun), 
Inter 
Milan wapo tayari kutoa pauni milioni 12 kumsajili winga wa Manchester 
United Nani (Daily Star), 
Mshambuliaji wa zamani wa Atletico Madrid 
Radamel Falcao huenda akawa anarejea tena Spain kujiunga na Real Madrid 
(Tuttosport), 
Manchester United wametoa pauni milioni 28 kumsajili 
kiungo wa Athletic Bilbao, Ander Herera (Marca),
 Juventus wameongeza dau
 na kufikia pauni milioni 14 kumwania Alvaro Morata wa Real Madrid, 
ambaye pia anasakwa na Arsenal (As.com). 
Hayo ndio yamedokezwa kwenye 
magazeti na mitandao Ulaya leo -tetesi nyingine kesho- panapo majaaliwa.

0 comments:
Post a Comment