Facebook

Tuesday 24 June 2014

Van Gaal: ''FIFA imetuonea''

Van Gaal akashifu FIFA kwa ratiba mbaya za mkondo wa pili
Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal amelishutumu shirikisho la soka duniani FIFA kwa "kufanya hila" kwa jinsi linavyopanga ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia.
Wenyeji Brazil walicheza mechi mbili kabla ya Uholanzi kucheza, lakini watacheza tena baada yake katika mechi ya mwisho ya makundi, jambo ambalo Van Gaal anadai sio la haki.
"FIFA inafanya hila hizi.
Sio jambo zuri," alisema Van Gaal ambaye  timu yake itachuana na Mexico katika mechi za mtoano.
"Sio mchezo wa haki.''
''Nadhani katika Kombe la Dunia taifa linaloandaa mechi hizi hutendekezwa ."
watakaomaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi A walioko Brazil watachuana na watakaomaliza katika nafasi ya pili katika kundi B siku ya Jumamosi, huku atakayemaliza katika nafasi ya pili katika kundi A akimenyana na atakayemaliza katika nafasi ya B siku itakayofuata.
"Brazil itachuana na Chile huku Uholanzi ikimaliza udhia dhidi ya Mexico"
Brazil waliilaza Cameroon 4-1.
Van Gaal ratiba zinapendelea Brazil.
Uholanzi na Chile tayari wamekwishafuzu lakini Uholanzi iliongoza kundi hilo, jambo ambalo limemfurahisha van Gaal ambaye amekiri kutaka kuepuka kucheza dhidi ya Brazil katika mechi ya kwanza ya raundi ya Mtoano.
"iwapo ningechagua mimi, nisingependa kucheza dhidi ya Brazil, ingawa Croatia na Mexico sio wapinzani dhaifu pia,".
Hata hivyo, kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari alisisitiza: "ni sharti tucheze ili kufuzu, sio kubaini na kuchagua wapinzani wetu. Ni FIFA ndio iliyochagua saa za kuanza michuano.
"kuna watu kadhaa waliotoa maoni kuwa tutachagua wapinzani wetu. ."
Maoni ya aina hiyo ya kipumbavu na nia mbaya
Mkufunzi huyo anayechukua hatamu Manchester United pia aliwashutumu marefa katika mashindano hayo, ambao alisema walizawadi penalti "zisizo za haki" dhidi ya timu yake katika mechi mbili za ufunguzi ambazo Uholanzi waliibuka washindi dhidi ya Uhispania na Australia.
Katika matukio yote mawili, timu pinzani zilifunga na kuwalazimu Uholanzi kutoka nyuma na kushinda.
"tumeona katika Kombe hili la Dunia kwamba penalti walizopewa wapinzani wetu katika matukio mawili hazikuwa halali, hilo ni sawa - angalau kwa maoni yangu," alisema.
"katiaka matukio mawili tunapata penalti. Hakuna taifa ambalo limewahi kushuhudia jambo kama hilo, kwa hivyo labda refa huyo [Bakary Gassama kutoka Gambia] atafanya kazi nzuri.
Ninatumai tu kwamba FIFA imefuata utaratibu mzuri wa kuchagua."

0 comments:

Post a Comment