Facebook

Friday, 27 June 2014

Man City yamsajili Fernando wa Porto.

Mchezaji wa Porto Fernando akimkabili ashley Cole wa Chelsea
Mabingwa wa ligi ya FA nchini Uingereza Manchester City wamemsajili mchezaji wa kiungo cha kati Fernando kutoka kilbu ya Porto kutoka Ureno.
Kilabu hiyo ya Porto ndio iliotangaza makubaliano hayo katika soko la hisa la Lisbon siku ya jumatano baada ya kukubali kumuuza mchezaji huyo kwa takriban paundi millioni 12.
City imethibitisha mpango huo siku ya alhamisi ijapokuwa maelezo ya makubaliano hayo hayakuwekwa wazi.
''Nitacheza uwezo wangu kila ninapokuwa katika uwanja na ninataraji kuichezea kilabu hiyo kwa miaka mingi ijayo.',alisema Fernando.
''Ninafurahia kuwa katika kilabu hii na natamani kucheza katika ligi ya Uingereza''.
Kwa mara ya kwanza mchezaji huyo alihusishwa na timu ya City mnamo mwezi January na ni mchezaji wa pili kusajiliwa na kilabu hiyo baada ya kumsajili beki wa kulia wa Arsenal Bacary Sagna.
''Nina furahi kujiunga na Manchester City'',aliongezea.Najua kulikuwa na mazungumzo ya mimi kusajiliwa na City mnamo mwezi January ,kwa hivyo ninafurahi kwamba makubaliano hayo sasa yameafikiwa na kwamba mimi ni mchezaji wa City.

Related Posts:

  • Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya. Fabio Borini, 23, anajiandaa kujiunga na Sunderland baada ya Liverpool kukubali ada ya pauni milioni 14 (Sky Sports), Baada ya kumchukua Filipe Luis siku ya Ijumaa, Chelsea wanazungumza na Atlètico Madrid kuhusu kums… Read More
  • UHAMISHO WA WACHEZAJI ULIOKAMILIKA HADI HIVI SASA LIGI KUU UINGEREZA KLABU za Ligi Kuu England zipo kwenye heka heka kubwa za kusajili Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu mpya wa 2014/15 unaoanza Agosti 16 lakini Dirisha la Uhamisho litafungwa rasmi Septemba 1 Saa 7 Usiku kwa saa za Afr… Read More
  • Nyota wa Nigeria asajiliwa West Brom.   West Brom wamemsajili mshambuliaji kutoka Nigeria Brown Ideye kwa kitita kinachodhaniwa kuwa pauni milioni 10. West Brom wametangaza kuwasili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akitokea Dynamo Kiev siku y… Read More
  • Algeria yateua kocha mpya.   Christian Gourcuff ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Algeria siku ya Jumamosi. Raia huyo wa Ufaransa anachukua nafasi ya Vahid Halilhodzic aliyewapeleka Mbweha wa Jangwani katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia … Read More
  • Mourinho "Nimemaliza Usajili"   Boss wa Chelsea, Jose Mourinho amesema amemaliza kununua wachezaji msimu huu baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kushoto Filipe Luis kutoka Atlètico Madrid. Luis ni mchezaji wa nne mpya kusajiliwa na Mouri… Read More

0 comments:

Post a Comment