Walimkosa nyota wa Brazil,
Neymar akiangua kilio wakati wimbo wa taifa wa nchi hiyo ulipokuwa
unapigwa katika mechi yao ya pili dhidi ya Mexico.
Wala hawana habari kuhusu penalti iliyozua utata katika mechi ya ufunguzi ya kombe la dunia.Hawa ni raia wa Brazil ambao hawana muda na kombe la dunia.
Badala ya kutizama soka kwa dakika 90 katika runinga zao, wanaona afadhali kuoka keki, kucheza baharini , kumtembeza Mbwa na kutizama vipindi wanavyovipenda kwenye televisheni au bora zaidi walale.
Victor Pavan, mwanafunzi mwenye miaka, 18,Sao Paulo
Sio rahisi kuwa raia wa Brazil sasa hivi hasa kama hupendi soka. Kwa sababu tu kwamba mimi ni mwanamume, kila mtu anadhani kuwa napaswa kufurahikia soka. Sijali wala sina muda wa soka. Hata siungi mkono timu yoyote ya nyumbani.
Mpenzi wangu ambaye ni shabiki wa klabu ya,Corinthians - anapenda sana soka.
Huwa naudhiwa sana nikisikia wati wakiongea kuhusu soka kwa muda mrefu. Mpenzi wangu anatazama mechi zote za kombe la dunia wakati mimi naona afadhali kuunga mkono filamu.
Wakati Brazil inapocheza, hata huwa siangalii ukurasa wangu wa Facebook kwa sababu kila mtu anaongea kuhusu kombe la dunia.
Hata siungi mkono nchi hii kuwa mwenyeji wa kombe la dunia. Yaani hili gumzo lote kuhusu kome la dunia linanichukiza kweli.
Lakini najaribu kabisa kutozungumzia kwa sababu kila mtu ana kitu ambacho anakipenda.''
Lucas Kanyo, Mbunifu mwenye umri wa miaka 39, kutoka Sao Paulo
Jumatatu wakati ambapo Brazil itacheza, mimi nitakwenda zangu kazini kama kawaida.
Wakati ambapo Brazil ilicheza dhidi ya Mexico Jumanne, nilihisi kuumwa, na kwa hivyo nikaamua tu kulala. Nililala mechi ilipokuwa inachezwa.
Sio rahisi kujiepusha na soka Brazil kwa wakati huu.
Ninapoingia kwenye Taxi, dereva anasikiliza mechi kuptia kwa redio. Nilishangaa sana nilipoamka , sikusikia milio ya fataki kwa sababu Brazil ilitoka sare tasa, lakini kwangu mimi nilihisi vizuri kwa sababu nilipumzika.
Kwa upande mmoja napenda kelele zote barabarani, msongamano wa magari na hayo yote hayanisumbui kwa sababu mimi hutumia baiskeli yangu.
Na kwa kweli, nilikuwa napenda kombe la dunia hadi, mwaka 1998 ambapo Brazil ilishindwa na Ufaransa mabao matatu kwa nunge. Baada ya hapo sijawahi kupenda tena soka.''
Roberta Milazzo, Menaja, mwenye umri wa miaka 42, Rio de Janeiro
Nilienda baharini wakati wa mechi za kwanza zilizohusisha Brazil, kama nilivyofanya tu wakati wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2010.
Wakati huo bahari huwa haina watu na wakati huo huwa ni mzuri sana kwangu.
Nchini Brazil, Kila kitu sasa kinahusu dimba la dunia, wakati michezo mingine haiungwi mkono. Kitu hicho kinanikasirisha sana.
Nilikasirika sana kuhusu hekaheka hizi zote za kombe la dunia.
Brazil inahitaji kuimarisha mambo mengi sana , sidhani kama soka ni moja ya mambo hayo.''
Elisa Nazarian, mwandishi, miaka 65 kutoka Sao Paulo
Hisia ambazo hutokana na michuano ya kombe la dunia hunigusa sana. Lakini punde baada ya mechi kuanza , mimi huzima televisheni. Sipendi soka sana.
Nakumbuka kusikiliza matangazo ya michuano ya kombe la dunia mwaka 1958 kupitia kwa redio. Hata nilitazama baadhi ya mechi, lakini mwaka 1970, hio ndio ilikuwa michuano ya mwisho kwangu kutazama.
Wachezaji wa siku hizi hawana msisimuko, hekaheka hizi zote za wachezaji ni kuhusu tu pesa.
Mimi nilitembeza Mbwa wangu wakati wa mchuano wa kwanza wa kombe hili la dunia. Sasa ndio wakati mzuri kwa sababu hakuna kelele kwani Mbwa huwa watulivu sana.
Mechi ilimalizika kwa sare tasa na hapakuw ana kelele hata kidogo.
0 comments:
Post a Comment