Wakili mashuhuri ambaye pia ni
mkereketwa wa haki za kibinadamu nchini Libya ameuliwa kwa kupigwa
risasi na watu wasiojulikana katika mji wa Benghazi nchini Libya jana,
Jumatano.
Mauaji hayo yametokea baada ya uchaguzi wa Wabunge - ambao wengi walidhani utapunguza visa vya utovu wa usalama.Salwa Bughaighis alishambulia nyumbani kwake jana jioni.
Ripoti kutoka Benghazi zinasema alishambuliwa na watu waliokuwa na bunduki waliokuwa wamefunika nyuso zao.
Matabibu kutoka hospitali ya Benghazi alikokufia walithibitisha kuwa alikufa kutokana na majeraha ya risasi aliyokuwa nayo kichwani.
Jamaa wake walisema kuwa majirani walimpeleka hospitalini na tangu wakati huo mumewe hajulikani aliko.
Jamii zake wanaamini ametekwa nyara ingawa haijulikani kwa hakika alivyotoweka.
Watu wengi waliosikia habari za kufa wakili huyo wameeleza masikitiko na hasira zao kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Alikuwa miongoni mwa mawakili wa kwanza na mkereketwa aliyepinga kutiwa mbaroni mara kwa mara kwa waandamanaji waliokuwa wakimpinga aliyekuwa mtawala wa Libya, Muamar Gadhafi.
0 comments:
Post a Comment