Facebook

Wednesday, 25 June 2014

Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini aachiliwa huru.

Mwanamke aliyeasi dini Sudan aponea

 
Meriam alihukumiwa akiwa mjamzito na kujifungulia gerezani

Wakili wake Elshareef Ali, amesema kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu
Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.
Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukata kukana kuwa yeye ni mkristo.
Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.
'Hamu kumuona mkewe'
Mumewe Meriam akiwa na wanawe wawili
Mumewe Meriam Daniel Wani, alisema kuwa ana hamu sana kumuona mkewe kwani taarifa hiyo ilitolewa bila yeye mwenyewe kuitarajia.
Amesema kuwa anataka familia yake kuondoka nchini Sudan haraka iwezekanavyo.
Wanandoa hao waliona kanisanmi baada ya kukutana mwaka 2011.
Hukumu ya kifo dhidi ya Meriam Yahia Ibrahim Ishag, ambaye alijifungulia gerezani, ilisababisha gadhabu sana hadi katika ulingo wa kimataifa.
"Tuna furaha sana kuhusu hatua hii ya serikalli na tunaelekea sasa kumchukua,'' alisema wakili wa Bi Meriam Elshareef Ali.
Bwana Ali alisema kuwa Bi Meriam alionyesha ujasiri mkubwa sana wakati huu wa masaibu yaliyomkumba.
''Ni ushindi kwa uhuru wa dini na imani, tunaamini kuwa katika siku za usoni hakuna mtu atakayelazimika kupitia masaibu kama yaliyomkumba Meriam,'' alisema wakili wake.
Babake Meriam alikuwa muisilamu ingawa mamake alikuwa mkristo na Meriam akaamua kuolewa na mwanamume mkristo.
Amekuwa gerezani tangu mwezi Februari pamoja na mwanawe mdogo.
Hata hivyo bwana Ali alisema kuwa hajaona hukumu ya mahakama ya rufaa na kwamba alipokea taarifa hizo kupitia kwa vyombo vya habari.

Related Posts:

  • Watu 10 wauawa katika mlipuko Nigeria   Ripoti kutoka kaskazini mwa Nigeria zinasema kuwa watu kadhaa wameuawa na mlipuko wa bomu karibu na mashine ya kutoa pesa ya ATM. Walioshuhdia walisema kuwa ,mwanamume mmoja alikaribia watu waliokuwa wamepanga fol… Read More
  • Wanajeshi wa Libya wafukuzwa Uingereza.   Wanajeshi kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa kimapenzi. Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni n… Read More
  • Je,wajua kuna waombolezaji wa kulipwa ?   Kila Alhamisi na Ijumaa, shughuli katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya, huvurugika kwa sababu mamia ya waendesha pikipiki huzuia barabara kutokana na kukodiwa kuomboleza msiba kwa malipo. Kelele za saut… Read More
  • Rais masikini zaidi duniani apewa dola milioni 1Rais wa Uruguay Jose Mujika anasema kuwa amepewa dola millioni 1 ili kuuza gari lake aina ya Volkswagen. Bwana Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha yake ,alisema kuwa ombi hilo lilitoka kwa kion… Read More
  • Obama aahidi kushirikiana na Republican   Kiongozi mpya wa Baraza la Senate la Marekani kutoka chama cha Republican na Rais Barack Obama wote wameahidi kumaliza mvutano wa kisiasa ambao umewavunja moyo wapiga kura wa Marekani. Wanachama wa Republican wa… Read More

0 comments:

Post a Comment