Facebook

Monday 23 June 2014

Wandishi wa Al Jazeera miaka 7 jela

Wandishi watatu wa Al Jazeera wamefungwa miaka 7 jela kwa kueneza habari za kupotosha
Mahakama nchini Misri imewahukumu jela miaka saba wandishi watatu wa habari wa shirika la habari la Al Jazeera waliokuwa wamezuiliwa kwa miezi sita nchini humo.
Walipatikana na hatia ya kueneza habari za kupotosha na kushirikiana na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Muslim Brotherhood.
Mmoja wa wandishi hao ni Peter Greste, raia wa Australia na ambaye pia alikuwa mwandihi wa habari wa BBC wakati moja.


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment