Wanajeshi wa Boko Haram wanaofanya mashambulizi na kuua raia wasio na
hatia huko Nigeria wamedaiwa kuanza kukimbia msitu baada ya nyoka wenye
sumu kali na nyuki kuwashambulia.
Habari hizi zilielezwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na kuthibitisha
kuwa ni mmoja wa member wa kundi la Boko Haram na alieleza kuwa hivi
sasa kundi hilo limelazimika kuhama msitu na linaelekea maeneo ya mpaka
wa Nigeria na Cameroon baada ya wanajeshi wake wa ngazi za juu
kushambuliwa na nyoka na kupoteza maisha.
Jeshi la Nigeria limeshafanya juhudi za kuwaondoa msituni lakini
imeshindikana na hadi sasa kundi hilo linawashikilia wasichana zaidi ya 260
na bado linaendelea kushambulia Nigeria kwa mabomu ya kutegwa.
0 comments:
Post a Comment