Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP, Dr. Reginald Mengi amekava jarida la Forbes Africa la mwezi July kama mfanyabiashara aliyefanikiwa zaidi kutoka kutembea peku hadi kuwa na utajiri wa zaidi ya $550 million (Barefoot to $550 Million).
Dr. Mengi ambaye December mwaka jana alitajwa na jarida hilo akishika
nafasi ya pili kama mmiliki binafsi wa vyombo vya habari tajiri Afrika
akimfuatia Koos Bekker wa Afrika Kusini, amezungumzia masuala ya uchumi
yanayohusu bara la Afrika.
Moja kati ya sehemu ya maelezo yake yaliyokaririwa ni pamoja na kueleza
kuwa bara la Afrika lina utajiri mkubwa lakini watu wake ni maskini.
“Africa as a continent is very rich but the people are poor.”
Jacquline Ntuyabaliwe aka K-lyn ambaye ni mama watoto wake mapacha amemuandikia ujumbe mzuri wa kumpongeza kupitia Instagram.
“Congratulations my love, you always make me so proud. I wish Jay and Ry were old enough to understand this now.”
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment