Aliyekuwa kocha wa Manchester
United David Moyes ameahidiwa kitita cha pauni milioni £4 kwa mwaka
ilikumrithi Roberto Mancini kama kocha wa Galatasaray ya Uturuki.
Iwapo mkataba huo utakubalika na ''The Chosen
one '' huenda raiya huyo wa Scotland akarejea katika safu ya ukufunzi
miezi michache tangu atimuliwe huko Old Trafford kufuatia msururu wa
matokeo duni.Galatasaray imedhibitishia waandishi wa habari kuwa Moyes alizuru Istanbul ilikufanya mkutano na rais wa klabu hiyo Unal Aysal.
Galatasaray, ilimaliza katika nafasi ya pili msimu iliokwisha nyuma ya Fenerbahce japo mabingwa hao wamepigwa marufuku ya kushiriki ligi ya mabingwa barani uropa kwa udanganyifu katika baadhiya mechi zao.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa vigogo hao wa ligi ya Uturuki Kufunzwa na Muingereza ,mwaka wa 1995 waliwahi kufunzwa na kocha Graeme Souness.
0 comments:
Post a Comment