Facebook

Monday 23 June 2014

Ghana yakana kupanga mechi Brazil


Rais wa shirikisho la soka nchini Ghana , amekanusha madai kuwa shrikisho hilo lilikubali timu ya Taifa kucheza katika mechi ambazo timu nyingine zilikuwa zinajiandaa kupanga.
Shirikisho hilo, pia limewataka polisi kuchunguza madai hayo.
Madai yenyewe yalitolewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na wandishi wa jarida la The Daily Telegraph.
"madai yaliyotolewa na gazeti hilo sio ya kweli,'' alisema Rais wa shirikisho la soka la Ghana GFA Kwesi Nyantakyi.
Shirikisho hilo limewataka maafisa wa polisi kuchunguza madai ya vyombo vya habari vya Uingereza kwamba mmoja wa maafisa wake alikubali timu ya nchi hiyo kucheza katika mechi zilizo fanyiwa ufisadi.
Mamlaka ya Soka nchini Ghana imekana madai ya jaribio lolote la kuuza mechi zake ama kuhusika kwa afisa yeyote katika ufisadi.
Madai hayo yametolewa kufuatia uchunguzi wa pamoja kati ya gazeti la Uingereza la Daily Telegraph na Runinga ya Channel Four.
Katika taarifa yake shirikisho la soka duniani FIFA limesema kuwa hakuna ushahidi kwamba uadilifu wa michuano ya kombe la dunia umeathirika.
Shirikisho hilo limesema kuwa litamuwekea vikwazo vikali afisa yeyote atakayepatikana na makosa hayo.


Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com

0 comments:

Post a Comment