Monday, 30 June 2014
TETESI ZA USAJILI NA KOMBE LA DUNIA
Mchezaji Roben ameomba msamaha kwa kitendo cha kujidondosha na kuzawadiwa penati iliyowavusha uholanzi hadi kufika robo fainali.
Klabu ya Real Madrid wametoa ofa ya E31mil kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling,
Vilabu vya Liverpool, Arsenal, Man United na Chelsea vipo katika rada ya kumuwania mchezaji Sami khedira kutoka Real Madrid (The Sun),
Liverpool wametoa ofa ya E 25mil mchezaji Lazar Markovic.
Liverpool wanatajia kutangaza leo au kesho asubuhi usajiri wa Adam Lallana ambaye alishafuzu vipimo siku ya ijumaa mchana.
Madrid wanasema kua wapo tayari kumuachia Di Maria kwa E 50 Mil na si vinginevyo (Daily Star).
Manchester United wanakaribia kumsajili William Carvaro kutoka Sportings, wapo kwenye maongezi ya kupunguza thamani ya E 36 mil ili waweze kupata huduma ya mchezaji huyo (O Jogo).
Liverpool wanamhitaji Iker Muniain kutoka Athletic Bilbao ila kikazo ni ada kubwa ya uhamisho wa E 45mil (AS).
Arsenal wana mpango wa kumsajili kinda la Southampton Morgan Schneiderlin mwenye thamani ya E 20 (Daily Mirror).
Liverpool wameomba FIFA imruhusu Suarez kufanya mazoezi na klabu wakati huu wa miezi minne aliyosimamishwa (Daily Express).
Liverpool wamepata upinzani kutoka Tottenham kwenye kupata huduma ya mchezaji Divock Orig (Daily Mirror).
Barcelona wanasema hawatishwi na mpango wa kumsajili L Suarezi kwa E 100Mil kwani wapo tayari kuitoa hiyo fedha na wanatoa hiyo ofa wiki hii baada ya kukubaliana na Suarezi mwenyewe (Daily Mail).
Manchester United Wapo tayari kutoa kitita cha E 6Mil kupata saini ya James Rodriguez ambaye wanatarajia kumpata mapema ( Guardian).
0 comments:
Post a Comment