Tangazo hilo ambalo limewekwa kwa mtindo wa bango katika eneo hilo lilisomeka hivi:
“Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, ILANI: Ni marufuku kufanya biashara na kuegesha magari katika eneo hili, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayevunja amri hii”.
Kamera ya Taarifa News ilikutana na bango hilo, pamoja na baadhi watu katika eneo ambao walikuwa wakijadili kuhusu tangazo hilo.
Taarifa News ilifanya jitihada za kuwatafuta viongozi wa eneo hilo bila mafanikio yoyote.
Kwa waliozoea kwenda Coco Beach na kula, bora mkaja na vyakula vyenu kuanzia sasa.
0 comments:
Post a Comment