Facebook

Saturday, 28 June 2014

Hofu imetanda katika kambi ya Brazil


Kocha wa wenyeji wa kombe la dunia Brazil, Luiz Felipe Scolari amekiri hofu imetanda katika kikosi chake baada yao kuratibiwa kuchuana na wapinzani wao wa jadi Chile katika mechi ya kwanza ya kundi la 16 bora itakayochezwa jumamosi.
Scolari aliyasema hayo katika mkutano na wanahabari kabla ya mechi hiyo.
Scolari alikiri kuwa hapa walikofika hakuna cha bahati na sibu kwani wakishindwa wataondolewa mashindanoni kwa hivyo hawana budi kujifunga kibwebwe dhidi ya wapinzani wao Chile.
Scolari; Hofu imetanda katika kambi ya Brazil
''Ninajua hofu na uwoga umetanda miongoni mwa wachezaji wangu lakini hilo linatarajiwa kwani hii ni Kombe la dunia nafkiri timu zote zilizofuzu kwa raundi ya pili zimejawa na uoga."
It is normal for us to be anxious, especially now in the knockout stage where we cannot lose," he said.
''Iwapo timu yeyote inataka kufuzu kwenye fainali ya kipute hichi hawana budi ila kushinda mechi zao.''
Brazil ilifuzu kwa mkondo huu wa pili baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare katika mechi moja ya makundi.
Scolari;Hofu imetanda katika kambi ya Brazil
Wenyeji hao wanamtegemea nyota wa Barcelona ya uhispania Neymar kuendelea na msururu mzuri wa kufunga mabao zaidi baada ya kuifungia Brazil mabao manne .
Kwa upande wao Chile walifuzu kwa mkondo wa pili baada ya kuzilaza Australia na mbingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania katika kundi B.
Wachambuzi wa maswala ya soka ya Brazil wanasema kuwa Scolari, huenda anahofia kushindwa na Chile .
Kocha huyo anasemekana kukiri hilo katika mahojiano punde tu baada ya droo ya kombe la dunia kufanyika mwezi Desemba.

0 comments:

Post a Comment