Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba ada ya uhamisho iliyotolewa na Manchester United inayokadiriwa kuwa kati ya Paundi milion 28 hadi 30 imekubaliwa na klabu yake ya Sothampton na anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo hii katika hospitali ya mashetani wekundu tayari kwa kujiunga na klabu hiyo.
Huku Patrice Evra akiwa ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja na Kuondoka kwa kinda mwingine aliyekuwa anacheza nafasi hiyo Alexander Buttner aliyekubali kujiunga Dyanamo Moscow mwanzoni mwa wiki hii kunatoa nafasi ya kinda huyo kujiunga na mashetani wekundu ambao tayari wameshaanza kuimarifa safu yao ya kiungo kwa kumsajili kiungo machachari kutoka Athletico Bilbao,Ander Herrera.
Akiwa maeonekana kwenye michezo 60 ya klabu ya Southampton Luke Shaw ataweka rekodi ya kinda aliyesajiliwa kwa dau la fedha kubwa zaidi duniani.Huku akiwa amemzidi kete aliyekuwa beki wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Ashley Cole na kuchukua nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa.
Luke Shaw alianza kucheza kwa mara ya kwanza katika timu yake ya Sothampton kutoka katika shule ya kukuzia vipaji ya klabu hiyo akiwa na miaka 16 mwaka 2012.
SOURCE:SKY SPORT
Imeandaliwa na.....
Katemi Methsela
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment