Siku chache baada ya kutokea shambulizi kubwa la bomu katika soko kubwa ‘Mall’ jijini Abuja, Nigeria mtoto mwenye umri wa miaka 13 amesaidia kuwaokoa raia wa Nigeria kushambuliwa na bomu kubwa baada ya kulishitukia na kutoa taarifa polisi.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Kano, aliyejitambulisha kwa jina la Magaji Majiya, mtoto huyo wa kiume alipata mashaka baada ya kuona gari fulani bovubovu likiwa limetelekezwa huku likiwa na mzigo mkubwa karibu na msikiti mmoja.
Na ndipo alipolichungulia na kuona vitu kama mabomu na akatoa taarifa mapema.
“Bomu liliwalenga watu walioenda kuabudu katika msikiti huo na lilikuwa limewekwa kwenye gari aina ya Toyota Tercel.” Alisema Majiya.
Polisi walituma kikosi maalum cha kutegua mabomu ambacho kilifanikiwa kulitegua bomu hilo.
Mtu mmoja amekamatwa kutokana na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment