Adokiye, 23, alitoa mapendekezo hayo kwa wanachama wa Boko Haram ili waweze kuwaachia huru wasichana wa Nigera wapatao 276 ambao waliwachukua mwezi Aprili katika mji wenye Wakristo wa kaskazini-mashariki wa Chibok.
Muimbaji na muigizaji huyo anayetokea jimbo la Imo aliliambia gazeti la Nigeria la Vanguard: ‘Hii ni saa 5 usiku, unajua ninachokifikiria?, wale wasichana wadogo, wako wapi saa hii, nini kitakuwa kinatokea kwao.
“Sio haki . bado ni wadogo. Natamani ningejitoa mimi tubadilishane.”
Balozi huyo wa amani wa Umoja wa Mataifa aliongeza: “Kuna wenye umri kati ya miaka 12 na 15. Nimekuwa na nina uzoefu. Hata wanaume 10 mpaka 12 wanaweza kunichukua kila usiku, sijali. Hebu waachieni hao wasichana, warudi kwa wazazi wao”.
Utekaji, ulioongozwa na kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, umeibua kampeni kubwa duniani ya #BringBackOurGirls. Imekuwa ikiungwa mkono na viongozi wakubwa kama David Cameron na Michelle Obama japo watumiaji wa Twitter hawana uhakika na manufaa ya ofa ya Adokiye.
Tumehamia
katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali
kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi
vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
0 comments:
Post a Comment