Facebook

Wednesday 27 August 2014

Arsenal yaghairi kusajili Mshambuliaji.


Arsenal hawana mipango ya kusajili mshambuliaji
mwingine kuziba pengo la Olivier Giroud - hata
kama vipimo vitaonesha ana jeraha kubwa.

Klabu
hiyo haina nia ya kusajili mchezaji yeyote wa
ushambuliaji kwa mkataba wa kudumu katika
dirisha hili la usajili.

Meneja wa Arsenal, Arsene
Wenger amesema atatazama kilichopo katika
soko la wachezaji wanaopatikana kwa mkopo.
Wenger anapanga kuwategemea Alexis Sanchez,
Joel Campbell, Yaya Sanogo, Lukas Podolski na
Theo Walcott.

Giroud alikuwa anapanga kukutana
na mtaalam ili kutathmini athari ya jerha lake,
alilopata katika mchezo dhidi ya Everton siku ya
Jumamosi uliomalizika kwa sare ya 2-2.
Kuna wasiwasi kuwa huenda amevinjika kiwiko
cha mguu na huenda akakosa kucheza kwa
karibu miezi mitatu.

Endelea kutembelea www.bantutz.com upate kilichobora.

0 comments:

Post a Comment