Facebook

Tuesday, 26 August 2014

Barcelona yaanza ligi kwa ushindi mnono..

Barca imefungua msimu kwa ushindi mkubwa dhidi ya Elche
Lionel Messi alifunga mabao mawili na kuisaidia Barcelona kuilaza Elche mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya mkufunzi mpya Luis Enrique .
Barca wangesajili ushindi mkubwa zaidi ila tu mchezaji mpya Munir aligonga mwamba sawa na Andres Iniesta.
Lionel Messi hakukosea alipofungia Barca bao la kwanza kunako dakika ya 42 chini kwa chini na kumpa kocha mpya Enrique sababu ya kutabasamu katika mechi yake ya kwanza akiwa kocha.
Sekunde chache baadaye Javier Mascherano alitimuliwa uwanjani baada ya kumchezea visivyo Garry Rodrigues.
Barca ilienda mapumzikoni ikiwa kifua mbele na ilirejea ikiwa na hamu ya kutamatisha ushindi huo.
Mashambulizi yalianza moja kwa moja na Munir El Haddadi alifungia Barca bao la pili kunako dakika moja baada ya kipindi cha pili kuanza.
Kuanzia hapo haikuwa siri vijana wa Enrique walikuwa na niya ya kufungua ukurasa mpya msimu huu.
Kocha Enrique ameimarisha kikosi chake kwa niya ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Messi alifunga bao lake la pili na kuihakikishia Barca Ushindi huo wa kwanza msimu huu.
Kwa kocha Enrique ambaye alimrithi Tata Martino, ushindi huu ulikuwa dalili ya mambo kubadilika baada ya Tata kuiongoza Barcelona kwa msimu wake wa kwanza ambapo walikosa kushinda taji lolote tangu mwaka wa 2007-2008.
Enrique aliwasajili wachezaji wapya Luis Suarez kutoka Liverpool, Ivan Rakitic kutoka Sevilla na Thomas Vermaelen kutoka Arsenal ilikuimarisha nafasi zake za kutwaa ligi na hata kombe la mabingwa barani Ulaya.
Kocha huyo alikuwa hata na wasaa wa kuwashirikisha wachezaji wapya Rakitic, kipa Claudio Bravo, mlinzi Jeremy Mathieu washambulizi wachanga Munir na Rafinha ilikuwa na uhakika wa utendakazi wao uwanjani.

Related Posts:

  • FIFA kuchunguza Mexico kwa ubaguzi Shirikisho la kandanda Duniani FIFA limeanza kuchunguza hatua ya kuiadhibu Mexico, baada ya madai kujitokeza kuwa mashabiki wake walihusika katika ma… Read More
  • Ecuador yailaza Honduras 2-1 Ecuador 2-1 Honduras Ecuador ilitoka nyuma na kubana Honduras mabao (2-1), katika mchuano wa kundi E, wa kombe la dunia uliochezwa katika uwanja wa Arena da Baixada huko Curitiba. Equador ilikua imeshindwa mabao… Read More
  • Yaya na Kolo Toure wafiwa na mdogo wao, Ibrahim Nyota wa Ivory Coast Yaya na Kolo Toure wametaarifiwa kuhusu kifo cha mdogo wao wakati wakiwa kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil. Ibrahim Toure alifariki siku ya Alhamisi mjini Manchester, akiwa na umri wa … Read More
  • Uingereza yaondolewa Brazil Uingereza imebanduliwa nje ya kombe la dunia Brazil. Uingereza wameondolewa kutoka kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil baada ya raundi ya kwanza, k… Read More
  • Uingereza 1- 2 Uruguay Suarez ashangilia bao lake dhidi ya Uingereza Uruguay wameilaza Uingereza 2-1 katika mechi yao ya pili ya kundi D. Luiz Suarez ndiye amefunga mabao yote mawili ya Uruguay Uingereza walikuw… Read More

0 comments:

Post a Comment