Facebook

Tuesday 26 August 2014

Mwanachuo amuua mwanae na kumuweka uvunguni.

 
Taarifa zilizotufikia hivi Punde kutoka Chimala.Mbalali mkoani Mbeya.
 Vena Mtati(27), mwanafunzi wa chuo cha Uuguzi Chimala-Mbalali, anashikiliwa na polisi kwa kosa la mauaji ya mtoto wake.
 

Vena alimuua mwanae na kumuweka kwenye mfuko wa rambo na kumtumbukiza kwenye "kisalfet" kisha kumuweka uvunguni mwa kitanda!
 

Tofauti na unyama wote huo Vena alimwagia chumvi mtoto huyo na vumbi la mkaa ili asininuke endapo atamtupa porini!"

Baada ya kukamatwa na kuhojiwa na polisi mwanafunzi huyo alidai kwamba amefanya hiyvo kwa sababu mwanaume aliyempa ujauzito na kumuahidi kumuoa alimtelekeza na kutimkia Dar es salaam.
 
     Hilo gunia ndo lina maiti ya mtoto!

Vena Mtati hivi sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi Wilayani Mbalali na kesi itapelekwa mahakamani.

 Imeandaliwa na.................
      Peter Bulimbe
     {Admin BantuTz}

0 comments:

Post a Comment