Facebook

Sunday 24 August 2014

Rapper maarufu ateleza jukwaani wakati akitumbuiza

 
Rapper IGGY Ame kuwa na mafanikio makubwa tangu mwaka jana,lakini alikuja kungundua siku ya Ijumaa "u-star" sio tu kuonekana vizuri na kuvutia.
Rapper huyo kutoka Australia alikuwa akiimba wimbo wake unaowika sana Fancy katika Avalon theatre ,Hollywood kama sehemu ya tamasha la pre-MTV VMAs ,Iggy aliteleza na kuanguka nyuma ya jukwaa hilo,ingawa alifanikiwa kurudi tena na kuendelea kutumbuiza.
Lakini haikuchukua muda kwenye mitandao ya kijamii kusambaa kwa tukio hilo kwani "hashtag Poor Iggy" ilianza kusambaa kwenye Twitter.


Mambo yanamwendea vizuri rapper huyo (24),aliyekua amevaa "top ya orange" na nywele za blonde alizozibana kwa nyuma ,ilikuwa katikati ya shoo kabla ya yeye kuteleza na kuanguka .Alionekana kutotambua kuwa alikuwa amekaribia mwisho wa stegi kwa nyuma hivyo kudondoka bila kutarajia,lakini alirudi vizuri juu ya stegi.


Katika hali ya kushangaza walinzi walionekana kwenda kumsaidia lakini alirudi ndani ya dakika chache na kuendelea na show,aliwaambia mashabiki wake "nashukuru sikuvunja miguu yangu"
Pia alikuja kuandika 

"Sorry but it would be a crime not to share this with you all, I know I laughed. #StillFinishedtheSongTho #KeptOnRapping #TheShowMustGoOn."
Tukio hilo lilishuhudiwa na wasanii wenzake waliokuwa backstage ,Rita Ora,Sam Smith na Charlie XCX.


               SamChris Swai
                {Admin BantuTz} 

0 comments:

Post a Comment