Facebook

Sunday 24 August 2014

Mtoto wa Kim Kardashian na Kanye West mwenye mwaka 1 aanza kutembea,aonekana huko San Diego.


Mtoto wa Kim Kardashian mwenye umri wa miezi kumi na tatu(13),North West aanza kutembea akiwa amevaa nguo iliyo chanwachanwa(ripped jeans) na vest nyeupe juu wakati wa matembezi huko San Diego akiwa na Mama yake, Kim Kardashian.
 
Kim(33) alionekana akimsaidia mtoto huyo aliyekuwa akitembea hatua zake za mwanzo tangu azaliwe wakati wa Outing LaJolla California.Katika matembezi hayo,dada yake Kim,Khloe Kardashian (35) na mama yao Kris Jenner (58) nao walijiunga wakitafuta hoteli kwa siku hiyo.
 
North alionekana kupendeza na ripped jeans ,ambayo Kim na Khloe hupendelea kuvaa jeans za namna hiyo,,juu alivaa vest nyeupe huku chini alivaa raba nyeusi zenye soli nyeupe.
Kanye West baba wa North hakuonekana katika matembezi hayo,ambapo familia hiyo ilionekana kwenda kumsalimia mama yake Kris Jenner ,Mary Jo aneyeishi karibu na pwan ya bahari ,kaskazini ya San Diego .

 

North alionekana katika jarida la CR fashion book mwanzoni mwa mwezi huu,,katika jarida hilo alivaa Sweta la Chanel na handbag pamoja na hereni nzuri,akiandikwa "a future fashion legend".
 

Kim alinukuliwa kipindi cha mwezi October akisema haya kuhusu mtoto wake
 "she has  a really cool,simple style,she likes sweet things that are not too frilly,she likes to be comfortable".Pia aliongeza "'I hope she will be into fashion, there will be nothing sweeter that the two of us getting ready together for the day.''
 

Imeandaliwa na..........
                                      Samchris Swai
                                     (Admin BantuTz)

0 comments:

Post a Comment