Facebook

Monday 25 August 2014

Dereva tax amrudishia mteja wake pesa zaidi ya Billion 2 alizosahau kwenye gari lake.

Dereva mmoja wa taxi nchini Singapore amepongezwa na kusifiwa kwa uaminifu na moyo wa imani baada ya kukabidhi kitita cha zaidi ya paundi 500, 000 sawa na mabilioni ya shilingi kilichokuwa kimesahaulika kwenye gari yake.
Dereva huyo Sia Ka Tian (pichani) mwenye umri wa miaka 70 na ambaye amekuwa akiendesha taxi katika mji wa Singapore kwa zaidi ya miaka 30, alikuwa amewashusha wapenzi wawili watalii kutoka Thailand waliokukwenda kujivinjari nchini humo, baadae aligundua katika kiti cha gari kuna mfuko mweusi ambao sio wa kweke.

0 comments:

Post a Comment