Facebook

Wednesday 27 August 2014

Tetesi za Usajili katika Magazeti mbalimbali barani Ulaya na BantuTz SPORTS.

Arsenal wapo tayari kutoa dau la pauni
milioni 50 kumtaka Edinson Cavani kutoka
Paris St-Germain, kutokana na Olivier Giroud
kuwa na uwezekano wa kutocheza kwa muda
mrefu kutokana na jeraha la mguu (Daily
Express),

Arsenal pia wanamtaka Danny
Welbeck, 23, kutoka Manchester United,
kuziba nafasi ya Giroud, lakini Man U
wanasita kumuuza Welbeck (Daily Mail),

Meneja wa Arsenal vilevile anataka kumchukua kwa
mkopo Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco,
na pia Loic Remy, 27, ambaye anapatikana
kwa pauni milioni 8.5 kutoka QPR (the
Guardian),

Meneja wa Manchester United Louis
van Gaal anafikiria kutaka kumsajili kiungo
wa Liverpool Joe Allen, 24, kwa kutoa pauni
milioni 20, (Daily Star),

United wanafanya
mazungumzo ya kumsajili Daley Blind, 24,
huku kipa wa zamani wa Man U, Edwin van
der Sar akiwa Manchester kukamilisha
uhamisho wa beki huyo wa Ajax (Daily Star),

Manchester United pia wanafikiria kumtoa
Shinji Kagawa, 25, au Javier Hernandez, 26,
kama chambo katika mkataba wa kumchukua
kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27,
(Independent),

Real Madrid watatumia kiasi
kikubwa cha fedha za mauzo ya Angel Di
Maria, kumnunua mshambuliaji wa Monaco,
Radamel Falcao (Le Sport),

AC Milan
wamethibitisha kuwa wanataka kuwasajili
Fernando Torres, 30, na kiungo Marco van
Ginkel, 21 kutoka Chelsea (Daily Express),

AC
Milan wamechoka kumsubiri Torres kuamua
anataka nini na wamempa makataa, huku
wakijiandaa kuanza kumfuatilia Roberto
Soldado, 29, kutoka Tottenham au Fabio
Borini, 23, wa Liverpool (Inside Futbol),

Tottenham wanajiandaa kukamilisha usajili wa
beki wa Sevilla Federico Fazio, 27, baada ya
kulipa pauni milioni 8 za kipengele cha
ununuzi (Daily Telegraph),

Spurs pia
wanafikiria kumfuatilia kiungo kutoka
Cameroon Alexandre Song, 26, ambaye
ameambiwa anaweza kuondoka Barcelona
bure (the Times),

Meneja wa QPR Harry
Redknapp yuko tayari kupanda dau kwa
kiungo wa West Ham Mohammed Diame, 27,
(Daily Mirror),

Alvaro Arbeloa anataka
kuondoka Real Madrid kabla ya dirisha la
usajili halijafungwa (El Chiringuito),

Manchester United wanajiandaa kutoa dau
jipya la pauni milioni 33.4 kwa Juventus
kumtaka Arturo Vidal (Gazzetta dello Sport),

Real Madrid watapambana na Barcelona na
Atletico Madrid kutaka kumsajili Marco Reus
kutoka Borussia Dortmund (AS),

Hatem Ben
Arfa anataka kubakia Newcastle licha ya
meneja Alan Pardew kutompanga (Newcastle
Evening Chronicle),

Arsene Wenger anataka
kumsajili mshambuliaji wa zamani wa
Birmingham City, Nikola Zigic ambaye ni
mchezaji huru ( www.zurnal.rs ).

Zimesalia siku
tano kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

0 comments:

Post a Comment