Facebook

Tuesday 26 August 2014

Manchester City yaigaraza Liverpool.

Epl: Matokeo na wafungaji wa mechi ya Liverpool vs Man City haya hapa
MABINGWA wa England, Manchester City, Jana Usiku wakiwa kwenye uwanja wao Etihad wameonyesha kuwa hawana mzaha walipoitandika Timu iliyomaliza Nafasi ya Pili Msimu uliopita, Liverpool,magoli 3-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England.
 
Hadi Mapumziko City walikuwa mbele goli 1-0 lililofungwa na Stevan Jovtic katika Dakika ya 41 baada ya mchezo safi mno iliyoshirikisha Wachezaji kadhaa wa City.
Katika Dakika ya 55, Jovetic tena alipiga goli na Sergio Aguero, alietokea Benchi, akafunga goli la 3.

Goli pekee la Liverpool lilikuwa la kujifunga wenyewe kupitia Zabaleta katika Dakika ya 83.

Kivutio kwenye Mechi hii alikuwa Mchezaji mpya wa Liverpool, Mario Balotelli, alienunuliwa kutoka AC Milan, akiwepo Jukwaani kwa Watazamaji akiingalia Timu yake mpya ikichapwa na Klabu yake ya zamani Man City.

0 comments:

Post a Comment