Facebook

Friday 29 August 2014

Tetesi za Usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya na BantuTz SPORTS.


>Meneja wa Manchester United Louis van Gaal
anajaribu kumnunua kiungo wa Juventus
Arturo Vidal, 27, na beki wa Ajax Daley Blind,
24, kabla ya dirisha la usajili kufungwa
Septemba mosi (Daily Mirror), United
watalazimika kulipa pauni milioni 20
kumsajili Blind (Sun),

>Liverpool bado
wanajaribu kumfuatilia kiungo wa zamani wa
Arsenal Alex Song, 26, ambaye yuko
Barcelona (Metro),

>Meneja wa Arsenal,
Arsene Wenger amesema hatotaka kuwasajili
Danny Welbeck, 23, kutoka Man U, Radamel
Falcao kutoka Monaco, 28, na Nikola Zigic,
33, kutoka Birmingham (London24.com),

>Manchester United watapanda dau la pauni
milioni 24 kwa kiungo wa Sporting Lisbon
William Carvalho, 22, wakati Louis van Gaal
akitaka kuwaondoa Welbeck, Tom Cleverly,
25, na Shinji Kagawa, 25 (Daily Telegraph),
Cleverly yuko tayari kusalia hadi mwaka ujao
mkataba wake utakapokwisha (Independent),

>Sunderland wametoa dau la pauni milioni 6
kumsajili beki Virgil van Dijk, 23, kutoka
Celtic baada ya Toby Alderweireld, 25 wa
Atletico Madrid kukataa kwenda kuichezea
Black Cats (Times),

>Mchezaji wa zamani wa
Juventus Allesandro Del Piero amekubali
kujiunga na Delhi Dynamos ya India baada ya
mkataba wake na Sudney FC kumalizika
(Football Italia),

>Crystal Palace wanajiandaa
kumsajili tena Wilfried Zaha kutoka
Manchester United baada ya Neil Warnock
kurejea kama meneja (Daily Star),

>kiungo wa
Real Madrid Xabi Alonso, 32 anakaribia
kujiunga na mabingwa wa Ujerumani Bayern
Munich kwa pauni milioni 8 (Guardian),

>Real
Madrid wanataka kumsajili Marco Reus lakini
wapo tayari kusubiri hadi msimu ujao (AS),

>Chelsea wamekubali euro milioni 12.5 kutoka
AC Milan kumsajili Fernando Torres (The
Sun),

>Borussia Dortmund wameonesha nia ya
kumrejesha Shinji Kagawa katika Bundesliga,
baada ya kushindwa kuwika akiwa Old
Trafford (Kicker),

>Maafisa wa Juventus
wamekutana na maafisa wa Monaco kujadili
suala la Radamel Falcao kwa mkopo (Gazetta
dello Sport),

>Inter Milan wanataka
kumchukua Xherdan Shaqiri kutoka Bayern
Munich, iwapo Ricky Alvarez ataondoka wiki
hii kwenda Sunderland (Corriere dello Sport)

>Diego Costa huenda akakosa kucheza kwa wiki
sita baada ya kuumia msuli wa paja (Daily
Telegraph).

Zimesalia siku nne kabla ya
dirisha la usajili kufungwa.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa mbalimbali za michezo kwa wakati na muda muafaka.

0 comments:

Post a Comment