Facebook

Wednesday 27 August 2014

Mtoto amuua Mwalimu wake kwa kumpiga risasi Marekani.


Msichana wa miaka tisa nchini Marekani
amemuua kwa kumpiga risasi, kwa bahati
mbaya, mwalimu wake aliyekuwa
akimfundisha jinsi ya kutumia bunduki.
Mwalimu huyo alikuwa akimpa mafunzo
msichana huyo katika kituo cha kupigia risasi
kilichopo Arizona, wakati msichana huyo
alipopoteza mwelekeo baada ya kufyatua
risasi ya kwanza, katika bunduki aina ya Uzi.
Mwalimu huyo, Charles Vacca, 39, alipigwa
risasi kichwani na kufariki wakati akipelekwa
hospitali kwa ndege mjini Las Vegas.
Msichana huyo alikuwa katika kituo hicho
pamoja na wazazi wake.
Ajali hiyo ilitokea Jumatatu iliyopita katika
kituo cha kupiga risasi cha Last Stop,
kilichopo White Hills, Arizona.
Waandishi wa habari wanasema ni jambo la
kawaida katika maeneo mengi nchini
Marekani kwa watoto kufunzwa jinsi ya
kutumia bunduki.
Vituo vingi vya kupigia risasi huwa vina
sheria kali za usalama hasa kwa watoto.
Haifahamiki kituo hicho kina kanuni zipi
kuhusiana na umri wa chini ambao watoto
wanaruhusiwa kuanza mafunzo.

0 comments:

Post a Comment