Facebook

Friday 29 August 2014

Tetesi za Usajili katika magazeti mbalimbali Barani Ulaya na BantuTz SPORTS

Real Madrid wamekamilisha uhamisho wa
pauni milioni 20 wa Radamel Falcao, 28,
kutoka Monaco (Calciomercato),

Arsenal
wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa
beki Sorkatis Papastathopoulos, 26, kutoka
Borussia Dortmund, lakini wamesema
hawatalipa pauni milioni 20 (Daily Mirror),

Meneja wa Aston Villa Paul Lambert ametoa dau
la pauni milioni 8 kumtaka kiungo wa
Manchester United Tom Cleverly, 25, (Daily
Telegraph),

Lakini Lambert huenda wakapata
upinzani mkali kutoka Valencia, ambao nao
pia wamepanda dau kwa Cleverly (Sky
Sports),

Danny Welbeck, 23, anajiandaa
kuondoka Old Trafford, na akitajwa kwenda
Tottenham kwa mkopo (Daily Star),

Chelsea
wanakaribia kutoa ruhusa kwa Fernando
Torres, 30, kwenda Inter Milan (Times),

Manchester United wameongeza bidii
kumfuatilia kiungo Martin Odegaard, 15,
anayechezea Stromsgodset kutoka Norway
(Daily Telegraph),

Valencia na Juventus
wametoa dau la kutaka kumsajili Javier
Hernandez, 26, kutoka Manchester United
kwa kiasi cha pauni milioni 15 (Guardian),

Mshambuliaji Demba Ba, 29, alikaribia
kujiunga na Arsenal kabla ya kusaini kwenda
Besitkas ya Uturuki kutoka Chelsea kwa pauni
milioni 8 (Independent),

kiungo anayesakwa
na Manchester United Arturo Vidal, 27,
amekaririwa akisema hataki kuondoka
Juventus (Daily Express),

kiungo wa zamani
wa Arsenal Alex Song, 26, ana matumaini ya
kurejea katika Premier League na Liverpool
baada ya Barcelona kuonekana kutomtaka
(Daily Mirror),

kiungo wa PSG Adrien Rabiot
ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao
anasakwa na Roma na Arsenal (Le Parisien).

Zimesalia siku tatu kabla ya dirisha la usajili
kufungwa.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze taarifa mbalimbali za Usajili barani Ulaya.

0 comments:

Post a Comment