Facebook

Tuesday 26 August 2014

Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya na BantuTz SPORTS.

>Boss wa Manchester United Louis van Gaal
anataka kumsajili kiungo wa Juventus Arturo
Vidal, 27, kwa mkataba wa pauni milioni 34
kiasi ambacho kitafikisha pauni milioni 200
za kununua wachezaji Old Trafford katika
kipindi cha miaka miwili (Independent),

>United huenda wakamtoa Javier Hernandez,
26, kwenda Juventus, katika mkataba wa
Vidal (Daily Express),

>Manchester United pia
wanatarajia kutaka kumsajili Daley Blind, 24
kutoka Ajax kwa pauni milioni 18 katika siku
chache zijazo (Sun),

>Arsenal wanaonekana
kuzidiwa kete na Roma, kumsajili beki wa kati
Kostas Manolas, 23 kutoka Olympiakos
(Goal),

>Manchester United na Arsenal
wamepata matumaini ya kuendelea
kumfuatilia beki wa Roma Mehdi Benatia, 27,
baada ya klabu hiyo ya Italia kuvunja
mazungumzo na Bayern Munich (Daily Star),

>Arsenal huenda wakamfuatilia Danny
Welbeck, 23, kutoka Man United, au Loic
Remy, 27, kutoka QPR kuziba pengo la
Olivier Giroud ambaye huenda akakosa
kucheza kwa miezi mitatu kutokana na jeraha
la kiwiko cha mguu (Daily Telegraph),

Southampton wameanza kumfuatilia beki wa
Atletico Madrid Toby Alderweireld, 25, na
kuwazidi Monaco (Times),

Tottenham wapo
tayari kutoa pauni milioni 8 kumchukua
nahodha wa Sevilla Federico Fazio, 27
(London Evening Standard)

>Chelsea
wanazungumza na Roma kumchukua Mattia
Destro, 23 (Daily Mirror),

>QPR wanakaribia
kumsajili beki wa Liverpool Jack Robinson, 20
kwa mkataba wa pauni milioni 1 (Daily
Mirror),

>West Ham wamemuulizia beki wa
kati wa Bayer Leverkusen Philipp Wollscheid,
25, (Daily Mail),

>Sunderland, QPR na West
Brom wanamtaka kiungo wa Leicester Andy
King, 25, (Sun),

>AC Milan bado wanataka
kumchukua Fernando Torres kutoka Chelsea,
wakala wake akipendekeza kumchukua kwa
mkopo, ingawa mshahara wake mkubwa
unaonekana kuwa kikwazo (Metro),

>Napoli
wataanza kumfuatilia tena kiungo wa
Tottenham, Sandro kwa mkopo (The Times),

>Sporting wamewaambia Arsenal kuwa
watakubali kitita cha euro milioni 30
kumsajili William Carvalho, kama Arsenal
watakubali kumtoa Serge Gnabry, Francis
Coquelin au Yaya Sanogo kwa mkopo (The
Times),

>Everton wanakaribia kukamilisha
usajili wa Samuel Eto'o. Roberto Martinez
alikuwa akimtaka Danny Welbeck wa Man
United, lakini alikatishwa tamaa na bei ya
Pauni milioni 15 (The Times) 

>Boss wa Inter
Milan, Walter Mazzarri amewaambia watu
wake kuwa wako huru kujaribu kumsajili
Ezequiel Lavezzi kutoka Paris St-Germain
(Tuttosport).

Zimesalia siku sita kabla ya
dirisha la usajili kufungwa.

0 comments:

Post a Comment