Serikali imeanza kuingiza nchini vifaa
vya kuwabaini watu wanaohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa homa kali ya
ebola ambavyo vitawekwa kwenye viwanja vya ndege pamoja na baadhi ya
maeneo ya mipakani.
Jana Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk Steven Kebwe alikabidhi mashine nne za kuwapima abiria
wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege bila kuwagusa. Vifaa hivyo
vinabaini mtu kuwa na dalili za ebola kutokana na joto lake na abiria
wanapimwa kwa kumulikwa machoni na kwenye masikio.
Kwa kuanzia mashine hizo ambazo ni mfano
wa kamera zitapelekwa kwenye viwanja vya ndege vya Mwanza,
Kilimanjaro, Zanzibar na Dar es Salaam. Maeneo hayo kwa mujibu wa naibu
waziri huyo ndiyo yanapokea wagonjwa wengi kutoka nje ya nchi.
Dk Kebwe pia aliagiza shehena ya mashine
zingine zitakazoingizwa nchini kuanzia leo zipelekwe kwenye viwanja
vingine vya Mtwara, Kigoma na maeneo ya mipakani kuhakikisha kuwa kila
abiria anayetoka nje ya nchi anapimwa dalili za ugonjwa huo hatari.
Pia aliagiza wanadiplomasia na viongozi
wa kitaifa wanaotoka nje ya nchi ambako wanakwenda kuhudhuria mikutano
mbalimbali pia wapimwe kwani ugonjwa hauchagui cheo wala fedha na hadhi
aliyo nayo mtu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa
(MSD), Cosmas Mwaifwani alisema jana kuwa wamenunua mashine hizo nne
kutoka Afrika Kusini, lakini zimetengenezwa nchini Marekani kwa kiasi
cha Sh milioni 16.
Alisema katika kipindi hiki ambacho kuna
mlipuko wa ugonjwa wa ebola huko Afrika Magharibi, upatikanaji wa vifaa
hivyo ni adimu na haiwezekani kupata mashine zote kwa msambazaji mmoja,
hivyo akasema leo ziwawasili mashine nyingine mbili kutoka Ubelgiji.
Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri
Mchunga alisema mashine hizo kitaalamu zinajulikana kama thermo scanners
ni mashine za mkononi na kila abiria atakayeshuka uwanja wa ndege
atapimwa kwenye macho au masikio bila kugusana.
Monday, 25 August 2014
Vifaa vya kuwatambua wenye EBOLA vyawasili Tanzania.
Related Posts:
Samwel Sitta ajitosa kuwania Uspika.Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta amechukua fomu za kuwania uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni,Ndugu Mohamed Seif Khatib… Read More
Rais Dkt Magufuli apokea hati ya makabidhiano ya Ofisi ya Ikulu kutoka kwa Rais Mstaafu Dkt Kikwete leoPicha:-Rais Dk MagufuliJP akipokea hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Dk J M. Kikwete Ikulu Dar leo. … Read More
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya apiga marufuku matumizi ya simu za mkononi wakati wa kaziMkuu wa mkoa wa Mbeya amepiga marufuku matumizi ya simu za mkononi wakati wa kazi mkoani Mbeya ili watumishi wa serikali na mashirika ya umma wahudumie jamii kwa wakati. Asisitizia marufuku mtandao wa WhatsApp, ataka wa… Read More
Rais Mstaafu J.M.Kikwete awaachia WaTanzania Ujumbe huu.Ikiwa leo Novemba 5, 2015 ndio Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemaliza muda wake wa kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Dk.John Pombe Magufuli akiapishwa kama rais wa awamo wa 5 wa kuliongoza taifa hili.Sasa kupi… Read More
Bantuz MAGAZETINI-Soma kilichoandikwa katika Magazeti ya leo Novemba 12. BantuTz MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusoma na kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata ha… Read More
0 comments:
Post a Comment