Facebook

Friday 29 August 2014

HEKIMA ZA KIIMBILA "MANCHESTER WANAPOJIFUNIKA KITAMBAA CHEUSI WAKATI WA JUA KALI"





Photo: Louis van Gaal hails Di Maria as a team player and believes he will succeed at United: “He can accelerate the game for us but he can also play in the interest of the team. That is what I like in Di Maria, not only his class.” 

More from the boss: http://bit.ly/1vqewT5    Naona sasa Manchester united wameamua kwenda Muhimbili na kupasuliwa kichwa wakati wao wanaumwa goti.

      Inasikitisha sana yani kwa jinsi walivyoshangilia ujio wa Angel di Maria ni kama vile hawana wachezaji wakubwa au pengine wachezaji wakubwa zaidi ya huyo,wapo wengi sana. 

 Photo: Robin van Persie returned to action for the Reds last weekend and we can’t wait to see what he can do this season. Watch his highlights and best goals from the last two years at United here: http://bit.ly/18yPo2B
Kagawa,Rooney,Juan Mata na Robin Van Persie wote hawa wana uwezo mkubwa na hata majina makubwa,tatizo hawa Red Devils wanaumwa kichwa lakini wameamua kwenda Muhimbili kupasuliwa goti sasa tusubiri tuone matokeo yake utasikia mara Edwood kapigiwa makofi mara anazomewa. 
Photo: Walking out last night as captain of Manchester United was an unbelievably proud moment for me and my family. It’s a huge honour for me to captain this great club and I will take great pride in doing so. I would like to thank all the fans for their support, I am looking forward to the exciting times ahead and leading their club to more success.
Manchester United wamefunika macho yao na vitambaa vyeusi yani wao hata mchana wanaona giza tatizo la timu yao hawalioni wanakimbilia kusajili majina makubwa.
 Photo: Welcome to Manchester United Marcos Rojo looking forward to playing with you.
Sawa bwana kwani mara nyingine uzuri wa mapambo huficha ubaya wa bibi harusi japo siyo siku zote. 
 
Hapo naanza kumkumbuka Sir Alex Ferguson kama daktari basi alikuwa daktari bingwa sana au mashuhuri kwani aligundua tatizo na kulifanyia kazi kwani alimchukua Robin Van Persie kutoka kwa jirani yake mmoja akiona kabisa kuwa alikosa ubingwa kisa hakuwa na mshambuliaji makini na wa uhakika. 
Photo: How many LIKES For Chicharito???
Mi naamini Chicharito hajawai kushuka wala kupanda kiwango lakini Chelsea walikuwa wakimwona akitokea bench basi suruli zao zilijaa maji, jasho na wengine hata mikojo, kwanini? 
 Sir Alex Ferguson
Hilo swali majibu yake anayao Ferguson akiwa ameketi nyumbani kwake au kwenye mashindano ya farasi hana habari kabisa ila majibu anayo. 

We unamkumbula Welbeck dhidi ya Real Madrid au mi sikuona naamini isingekuwa kadi Nyekundu ya shujaa wa siku hiyo na muoga wa leo Luis Nani basi Manchester United wangempiga yule jamaa.

Rafael Da Silva- The Brazilian Beast        Tazama hii Rafael, Evra, Vidic na Ferdinand sawa hata kama watu wanazeeka au wanafulia ila usingepita kirahisi kwenda kufunga goli wakati nje Ferguson kakaa pale kwenye bench fundi peke yake fundi mwenyewe.
 Photo: Louis van Gaal blames "big errors” in the build-up to MK Dons' goals but encourages fans to stick by the Reds: “Of course it’s very disappointing; I hope they maintain their confidence in the club and in our philosophy because that philosophy takes time.”
 Mi naamini Luis Van Gaal baba yake na Robben, Sneijder, Van Persie na Huntelaar ni kocha mzuri ila naomba tu mniruhusu nimnyanganye kitambaa cheusi walichovaa mashabiki wake ili yeye asione giza na nimkataze kwenda Muhimbili asije akapasuliwa kichwa wakati yeye ni mgonjwa wa goti.
    
       Imeandaliwa na..........

                                             Kelvin Kiimbila Ngote Jr.
                                        {BantuTz CABINET MEMBER}
                                               {+255719580495} 
                                              
Ni muendelezo wa BantuTz kuinua vipaji mbalimbali vilovyojificha,kama unauwezo wa kuandaaa makala makini na zenye mantiki usisite kuwasiliana +255716418657

0 comments:

Post a Comment