Facebook

Monday 25 August 2014

SIMEONE AFUNGIWA MECHI NANE


Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone
amefungiwa mechi nane kwa utovu wa
nidhamu alioonesha kwenye mechi ya Spanish
Super Cup. Simeone, 44, alimgusa mmoja wa
waamuzi kisogoni katika mechi iliyokuwa
imejaa hamasa kati ya Atletico Madrid na
Real Madrid, ambapo Atletico walishinda 2-1.
Shirikisho la soka la Spain (RFEF)
limethibitisha kuwa adhabu hiyo ni ya
makosa manne tofauti. Kocha msaidizi
German Burgos atasimamia mechi za
Attletico wakati wa adhabu hii.

0 comments:

Post a Comment