Facebook

Tuesday 26 August 2014

Mtu aliyekufa;afufuka Brazil.

Bwana mmoja nchini Brazil ameibuka saa mbili baada ya kutangazwa kuwa amekufa.Mtu huyo mwenye umri wa miaka 54
Valdeluco de Oliveira, ambaye alikuwa anaugua saratani alipelekwa hospitali baada ya kulalamika kusumbuliwa na matatizo ya kupumua. Kikosi cha madaktari katika jimbo la kaskazini mashariki la Bahia kiliwaambia ndugu zake kuwa bwana de Oliveira alikuwa amekufa baada ya kupata mishtuko miwili ya moyo. 


Ndugu hao walisaini cheti cha kifo na kuupeleka mwili wake katika chumba cha kuhifadhi maiti. Saa mbili baadaye, wafanyakazi wa hospitali waliona mwili wa mtu ukitikisika na kwenda haraka kumsaidia.Hospitali hiyo, katika mji mkuu wa jimbo la Salvador imeanzisha uchunguzi juu ya suala hilo. Mama wa Bwana Oliveira amesema maombi yake ya maajabu kutokea,yamejibiwa.

0 comments:

Post a Comment