Facebook

Sunday 31 August 2014

Tambwe afungua akaunti ya magoli.

Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu
uliopita, Khamisi Tambwe ameanza kuonyesha
makali baada ya kupiga bao mbili katika
mechi ya jana usiku Simba ilipoiadhibu
KMKM ya Zanzibar kwa mabao 5-0.

Tambwe raia wa Burundi alipiga bao mbili na
kuiwezesha Simba kuongoza kwa mabao 4-0
hadi mapumziko kwenye Uwanja wa Amaan,Zanzibar.

Wengine waliofunga mabao ni wakongwe
Amri Kiemba na Shaaban Kisiga ambaye
alipiga bao zuri sana baada ya kupokea pasi
ya Tambwe.

Kipindi cha pili, Elius Maguri naye alipiga bao
la tano huku wanachama wa kundi la Friends of
Simba (Fos) wakishuhudia uwanjani hapo.
Simba ilionyesha soka safi na la kuvutia
katika kipindi cha kwanza lakini ikaendelea
kuwapa kazi KMKM katika kipindi cha pili
huku ikitumia vijana zaidi.

0 comments:

Post a Comment