Facebook

Thursday 28 August 2014

Rooney ateuliwa kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza


Mshambuliaji wa Manchester United Wayne
Rooney ametajwa kuwa nahodha wa timu ya
taifa ya England, na meneja Roy Hodgson.
Rooney, 28, anachukua nafasi iliyoachwa na
Steven Gerrard aliyestaafu, baada ya England
kutolewa katika michuano ya Kombe la
Dunia. Rooney ambaye amefunga magoli 40
katika mechi 95 alizocheza England, pia
alitajwa kuwa nahodha wa Manchester
United na Louis van Gaal mapema mwezi
huu.
"Ni kitu ambacho nitajivunia kukifanya.
Kuteuliwa kuwa nahodha ni kitu ambacho
hata sikuwahi kukiota." amesema Rooney
katika tovuti yake rasmi.

0 comments:

Post a Comment