Facebook

Saturday 30 August 2014

"El Nino" ajiunga AC Milan.

Fernando Torres ameondoka Stamford Bridge
na kuhamia San Siro.
Straika huyo atakua AC Milan kuziba pengo la
Mario Balotelli baada ya mu-Italiano huyo
kujiunga na Liverpool kwa ada ya £16m.
Torres na Chelsea wamwfikia makubaliano
hayo ya kukatisha mkataba wao wa miaka 5
na nusu, baada ya straika huyo kuitumikia
The Blues bila mafanikio kwa miaka mitatu na
nusu.
Amesaini mkataba wa miaka miwili na AC
Milan kama mchezaji huru huku ikiaminika
Chelsea imemlipa kiasi cha pesa ili
kuhitimisha mkataba wake uliokua ukimlipa
£150,000-kwa-wiki kwa kua alisalia na miaka
miwili mkataba huo kumalizika.
Torres ameifungia Chelsea bao 45 tu katika
michezo 172 tokea kusajiliwa kwa ada ya
£50milioni akitokea Liverpool.

0 comments:

Post a Comment