Facebook

Tuesday 26 August 2014

Justin Beiber na Selena Gomez wahusishwa na wizi wa simu katika mgahawa.


Polisi waliitwa katika eneo la mgahawa wa Dave & Buster's ambapo Justin Beiber na "on/off girlfriend" Selena Gomez walionekana na hivyo kuhusishwa na tukio la wizi wa simu.

Watumiaji wa mtandao wa Twitter waliandika kuwa waliwaona Justin Beiber na "on/off girlfriend" Selena Gomez katika mgahawa huo siku ya jumatatu kabla ya tukio hilo la wizi kutokea .Msemaji wa polisi wa Los Angeles (LAPD) alithibitisha kuwa maofisa wa polisi waliitwa katika eneo hilo la mgahawa na michezo mingine muda wa saa 9:30 usiku baada ya mtu kuripoti mtu kutoka kundi la Justin Beiber kujaribu kuiba simu.

Polisi walisema ni kweli Mwimbaji Justin Beiber alikuwepo lakini kuhusu wizi lilikuwa ni la ujinga tu,kwani hakuna ugomvi wowote uliokuwepo wala vurugu zozote.Kama muda wa saa 1 kabla Justin Beiber alipost picha katika Instagram akiwa studio na mwimbaji wa R&B,Khalil na ilionekana akifurahia kuwa na on/off girlfriend wake.


Baada ya tukio hilo kuanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari,Justin Beiber alipost akicheza game ya Arcade kuonesha kuwa alikuwepo katika mgahawa huo.Pia mgahawa huo ndio ilikuwa unafunguliwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kutumika ndipo tukio hilo lilipotokea.


Mwezi Mei iliripotiwa na msichana mmoja kwa LAPD polisi,kuwa mwimbaji Justin Beiber alipokonya simu yake katika eneo la San Fernando course kwa kudhani alikuwa akimpiga picha mwimbaji huyo.Ingawa baadae madai hayo yalifutwa.

Justin na Selena walianza mahusiano mwaka 2010 lakini yamevunjika mara kibao.Kipindi cha karibuni imeripotiwa kuwa wanajifunza masomo ya Biblia kuwasaidia kuungana tena.

 

Picha aliyopost Justin Bieber akiwa na mwenzake Khalil studio,kabla ya tukio kutokea
 

       Mgahawa wa Dave & Buster's tukio lilipotokea
 

Justin Beiber alipost akicheza arcade game katika mgahawa huo

Imeandaliwa na.....
                          SamChris Swai 
                                             {Admin BantuTz}

0 comments:

Post a Comment