Facebook

Monday 25 August 2014

Chris Brown anusurika kifo Club;Suge Knight apigwa risasi.


Chris Brown amekoswakoswa kupigwa na risasi akiwa Club katika show ya pre-party ya usiku wa MTV VMAs . 
Mashahidi wanasema mwimbaji huyo Chris brown (25) alikoswa na risasi katika tukio hilo lililotokea klabu ya 10AK ,West Hollywood ambapo Chris Brown alikuwa kama mlengwa wa tukio hilo,wakati yeye akiongoza shoo ya pre-party ya usiku wa MTV VMAs .

 SUGE KNIGHT APIGWA RISASI


Mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya muziki
ya Deathrow ya Marekani na
mtayarishaji wa muziki Suge Knight
ameripotiwa kufanyiwa upasuaji katika
hospitali ya Cedars Sinai kufuatia kupigwa risasi katika sherehe isiyo pre-party ya usiku wa MTV VMAs ..
Suge Knight inadaiwa alipigwa risasi kadhaa mapema siku ya Jumapili usiku (Agosti 24), akiwa West Hollywood nightspot 1 Oak. Knight aliweza kuondoka huku akitembea mwenyewe
katika sherehe hiyo iliyoandaliwa na Chris Brown, kabla ya polisi kumsaidia


  
 

Katika party hiyo Justin Beiber,Rapper The Game na mwanamuziki Apple de Ap pia walikuwepo ambapo Chris Brown alikuwa akiongoza sherehe hiyo.Watu waliohusishwa na tukio hilo walihojiwa na polisi waliofika eneo hilo na kufunga barabara zote zinazoelekea katika klabu hiyo,huku pia watu waliohudhuria nao wakihojiwa kuhusu tukio hilo.

Wakati tukio hilo likitokea,Chris alionekana akipanda juu ambapo ni kama bar,huku akiwaambia watu wasiinuke.
Knight ni mtu ambaye amekuwa si mgeni katika matukio ya vurugu za kutupiana risasi .Rafiki yake Tupac Shakur alipigwa risasi mara 7 katika tukio la lilitokea barabarani Las Vegas ,septemba 1996 ,pia mwezi Mei Suge aliripotiwa akisema muuaji wa Tupac hajapatikana mpaka leo kwa sababu Tupac hajafa na anaishi kisiwani.
Pia Suge Knight alijeruhiwa na risasi mguuni katika tukio lililotokea katika sherehe za pre-party ya VMAs mwaka 2005,iliyokuwa ikiongozwa na rapper Kanye West.



Muda kidogo baadaye Chris Brown ali tweet kupitia account yake kama unavyoona hapo juu
 
Justin Beiber na The Game pia walikuwepo katika party hiyo!!
Chris Brown akiwa anafurahia na rafiki zake kabla ya tukio hilo kutokea.
          Imeandaliwa na......
                                        SAMCHRIS SWAI
                                         {Admin BantuTz}

0 comments:

Post a Comment