Facebook

Wednesday 27 August 2014

Gari linalojiendesha lenyewe lafanyiwa majaribio huko Japan,


nissan 3Taarifa ikufikie kutoka Samukawa, Kanagawa Japan ambako stori kubwa leo ni kampuni ya Nissan kupata furaha kubwa baada ya kufanikiwa kwa jaribio la gari walilolitengeneza ambalo linajiendesha lenyewe.
Unaambiwa limetembea umbali wa kilometa 2.3 likijaribiwa kwenye mikikimikiki ya aina mbalimbali barabarani kama vile kuovertake, kufata alama za barabarani, taa za kuongozea magari na hata sehemu za watu kuvuka barabara.YMo_system_rear_0826Nissan wamesema wanalengo la kuanza kuliuza hili gari miaka saba kutoka sasa, hiyo itakua mwaka 2020 ambapo gari hili lina kamera maalum pamoja na sensors zinazofanikisha kulipa taarifa ya tukio husika kwa wakati huo ndio maana linaweza kufanya kama inavyotakiwa mfano kushika breki, kukanyaga mafuta na vitu vingine.
  nissan 4
Kingine cha kushangaza, kwa mfano kwenye miji mikubwa ambayo parking ni tatizo unaweza kuliacha likajiendesha lenyewe kwenda kutafuta parking wakati wewe unawahi mahali alafu ukimaliza shughuli zako unalikuta linakusubiri likiwa limepaki vizuri kabisa.

0 comments:

Post a Comment