Manchester United wamekubali kutoa pauni
milioni 59.7 kumsajili Angel Di Maria kutoka Real
Madrid, na kuvunja rekodi ya uhamisho ya
Uingereza.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 26,
yuko mjini Manchester na atafanya vipimo vya
afya siku ya Jumanne, kabla ya kukamilisha
uhamisho ambao, ukithibitishwa utafikisha pauni
milioni 132 zilizotolewa na Manchester United
msimu huu kusajili wachezaji.
Huenda Di Maria akacheza mechi yake ya kwanza
dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi, mchezo wa
ligi kuu.
Ada hiyo itazidi rekodi ya uhamisho ya Uingereza
ya pauni milioni 50 zilizotolewa na Chelsea
kumchukua Fernando Torres kutoka Liverpool
mwaka 2011.
Manchester United mara ya mwisho walivunja
rekodi ya Uingereza ya uhamisho mwaka 2002
walipotoa pauni milioni 29.1 kumsajili Rio
Ferdinand kutoka Leeds United.
Tuesday, 26 August 2014
Manchester United yavunja rekodi ya Usajili kwa Di Maria.
Related Posts:
LIVERPOOL KUMTOA SADAKA LAMBERT ILI WAMNASE BENTEKE.KLABU ya Liverpool iko tayari kumtoa Rickie Lambert ili waweze kumsajili Christian Benteke kutoka Aston Villa. Mshambuliaji huyo ni mmoja kati ya nyota waliopo katika mipango ya usajili wa Liverpool majira haya ya kiangazi na… Read More
Falcao arudi rasmi Monaco. Klabu ya Manchester United imedhibitisha kuwa mshambuliaji waliye mchukua kwapo toka timu ya Monaco RADAMEL FALCAO atarudi monaco.Kocha wa Man United Luis Van Gal akiongea alisema "FALCAO ni mchezaji wa hali ya juu na mtu… Read More
BRENDEN RODGERS:WAMILIKI NDIO WENYE MAAMUZI JUU YANGU.Huku Mashabiki wakipandwa na jazba kwa Timu yao kubamizwa Bao 6-1 na Stoke City hapo Jana, Meneja wao Brendan Rodgers amesema ataondoka Liverpool ikiwa Wamiliki wake watataka hilo. Jana huko Britannia Stadium Liverpool waliaa… Read More
SIMBA WAJIBU MAPIGO KWA YANGA BAADA YA KUMNASA KIUNGO PETER MWALYANZI KUTOKA MBEYA CITYWAKATI Yanga SC wakisherehekea saini ya winga Deus Kaseke, Simba SC nao wamefanya yao mchana huu. Kiungo hodari mchezeshaji Peter Mwalyanzi kutoka timu ile ile, Mbeya City aliyotokea Kaseke amesaini Mkataba wa miaka miwili ku… Read More
HUENDA VIDAL AKATUA ARSENALKLABU ya Arsenal, imeripotiwa kupanga muda wao kwa ajili ya kutangaza usajili wanyota wa Juventus, Arturo Vidal. Vidal alikuwa katika mipango ya usajili ya Manchester United kiangazi mwaka jana lakini walikatishwa tamaa kufua… Read More
0 comments:
Post a Comment