Facebook

Sunday 31 August 2014

Lady Jay Dee afunguka baada ya kuzushiwa kutoka na "Serengeti Boy"

Baada ya kuzushiwa kutoka kimapenzi na kijana mdogo "serengeti boys" na gazeti moja kubwa nchini linaloongoza kwa udaku,Lady Jay Dee kupitia ukurasa wake wa Facebook akanusha taarifa hizo.

Akiwa katika hali ya kusononesha sana na kuhuzunishwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini vinavyofanya kila njia ya kumchafua na kuharibu taswira yake katika jamii.

Jay Dee almaarufu kama "KOMANDO" aliiandika hiki kupitia ukurasa wake wa facebook....

"Zamani ilikuwa haipo sehemu ya kujitetea,
gazeti likishaandika ndio limeandika.
Lakini sasa ulimwengu umebadilika, sio muda
wa watu wote kulishwa chakula kisichofaa.
Kwanza hicho kichwa cha habari kimenivunjia
heshma sana
Nafikiri lengo ni kuilazimisha jamii
inayomuelewa JayDee tofauti imuone kuwa ni
mtu asiefaa, sawa.
Dogo anaswa na mkoko? Huo mkoko
mmemnasa nao wapi wakati hizo picha ni
mimi nilizi post mwezi February
Instagram?????
Picha ambazo zilipigwa Nyumbani lounge
tena kutumia simu ya Gardner.
Jide, dogodogo gumzo mjini ��������
Gumzo ni kitu kinachoongelewa sana na
kilichoenea kila kona ,,,,,sasa hii habari ni
gumzo wapi ambapo haisikiki, ......
Mngeandika tumeamua kumuanzishia Jide
gumzo hili, ndio ningewaelewa.
Vitu vya kuzua.
Ni watu wengi tu wakija band wakipata nafasi
wanaomba kupiga picha na mimi na wengine
pia wanaomba kupiga picha na gari sababu
wanaipenda.
Kama mtu yoyote anavyoweza kupiga picha
na sanamu la kitu chochote anachokipenda.
Hivi je! Wimbo wa JayDee mgumba, JayDee
tasa umechuja? Umeisha chati?? Nashangaa
na najiuliza tu
Inawezekana wimbo huo umechuja ndio
maana mnatafuta wimbo mwingine utakao
hit zaidi ya ule
Ndio kinachopelekea kuandika story za
namna hii ����������������
Sio nyinyi mliokuja kuomba radhi kwa yote
mliowahi kuniandika na kudai kuwa
mmejirekebisha, miezi kadhaa tu iliopita?
Sio boss wenu aliemfuata Gardner na
kumwambia tumalize tofauti zetu?
Kama hizo tofauti zilikuwepo ������
Inawezekana nyie ndio mna tofauti na mimi,
sijawahi kuwa na tofauti na mtu hata
nisiemfahamu. ..
Nashukuru Mungu nilikataa msamaha wenu
ni kama nilihisi hamkumaanisha
Au sababu sijawahi kukubali show mlizotaka
kufanya na mimi?
Je! Hiki ni kisasi? Sielewi
Mungu alienisimamia ataendelea
Hii sio vita ya kwanza wala ya mwisho
Dunia ni mapambano.
Kama nia ni kufanya niishi maisha ya uoga,
kudhoofika na msongo wa mawazo
mmefeli ,,,,, wengine mkijidai ni wacha
Mungu huku mkiumiza nafsi za watoto wa
binadamu wenzenu.
No wonder mnaishi bila amani mbali na
utajiri mlionao kwa kuogopa visasi.
Sikuzaliwa kukata tamaa
Pia wapo wanaopenda kuandikwa kwenye
hayo magazeti yenu
Wafanyieni favor ya kuwapa hiyo nafasi mi
sifanyi muziki wa magazeti ya udaku
Mkiachana na mimi nitashukuru sana
Hata ndoa yangu ikivunjika haimaanishi
mnitafutie story za kunichafua
Ndoa ya Madiba ilivunjika sembuse yangu
nina utofauti ipi na binadamu wengine?
Nyie ndoa zenu ziko perfect si ndio?
Hewala watakatifu nyie, mnaoficha yenu na
kutangaza ya wenzenu.
Mwisho nawaomba watu mnaonielewa
kutoamini tu habari yoyote ambayo haijatoka
kwangu wala kwa muwakilishi wangu ambae
ni "Webiro Wakazi Wasira".
Kama kuna chochote cha watu kujua
nitakiongea mimi kwa mdomo wangu sio
kuwekewa maneno mdomoni.
Kila siku ooooh tulimpigia simu hapatikani,
namba yangu yenyewe kwanza hata
mnaijua???
Mngekuwa mnaijua msingekuwa mnahangaika
mnawapigia watu wangu wa karibu
kunitafuta , na hao watu hawawezi kunisaliti
ndio sababu mpaka miaka 70 mtaishia
kusema tulimpigia simu JayDee hapatikani.
Nyie muongee chochote mnachojiskia
Ila sie hatuna haki kujitetea ??
Hili nalo litapita kama mengine
Na inshallah nitakuwa hapa hapa
nimesimama nawaangalia
Picha moja wapo ni hiyo ambapo mtoto wa
vitoto alikuja siku hiyo hiyo na akapiga picha
na Gardner, mbele ya gari hiyo hiyo
mnayodanganya watu kuwa mmemkuta nayo
na mahala ni hapo hapo Nyumbani
Lounge, ,,,,, na picha nyingine ni hizo
nilizowahi kuzi post mimi mwenyewe mwezi
february leo zinanihukumu
endeleeni kudanganya jamii
Na hizo ni chat alizoniandikia huyo mtoto wa
vitoto ambae ndio ilikuwa mara yangu ya
kwanza kumuona na sijawahi kumuona tena. .
Zaidi ya kuongea nae twitter ,,, sisemi kama
mimi malaika lakini
Ukweli huwa hauchanganywi na uongo
Kwa hili mmenidhalilisha sana
Kama nia yenu jamii inione mwanamke
nisiefaa na ninaependa dogodogo
Basi Mungu atawaonyesha ukuu wake.8+**7"

Itakuwa ni jambo jema sana kwa "blogs" au chombo chochote cha habari kutokuandika taarifa yoyote kwa nia ya kumuharibia au kumchafua msanii au mtu falani katika jamii kwa msalahi ya mtu au watu fulani.

Sisi kama BantuTz tunaahidi hatutoandika habari yoyote isiyo na ukweli halisi.Ni wajibu wetu kukuletea habari iliyo haririwa vizuri pasipo mmpendelea au kumkandamiza mtu yeyote yule.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata habari za muhimu,za uhakika na zenye mantiki.

Imeandaliwa na........Katemi Methsela.

0 comments:

Post a Comment