Mlinzi Marcos Rojo aliyesajiliwa Manchester
United kutoka Sporting Lisbon ya Ureno
anakabiliwa na shauri la jinai kwao Argentina,
na
ndilo linamzuia kuanza kuchezea timu yake
mpya. Hadi Jumapili hii asubuhi alikuwa
hajapatiwa visa ya kumwezesha kufanya kazi
nchini, kutokana na madai kwamba ana kesi ya
jinai ya kupigana na jirani nchini Argentina
tangu
2010 ambayo bado ipo kwenye majalada ya
polisi. Rojo (24) alikamilisha usajili kwa dau la
pauni milioni 16 wiki mbili zilizopita, lakini
upelelezi wa vitendo vyake vya jinai
unasababisha zuio la yeye kupewa visa, walau
kwa muda huu, japokuwa Kocha Mkuu wa Man
U, Louis van Gaal anasema ana uhakika
mchezaji huyo atakuwa tayari kwa mechi dhidi
ya Queen Park Rangers (QPR) Septemba 14.
Imeelezwa, hata hivyo, kwamba Chama cha
Soka
(FA) cha England kimeshamalizana na suala la
mtu huyo wa tatu na kimetoa hati ya
kumwezesha kucheza, lakini kinachosubiriwa
sasa ni visa, kwani aliyoingia nayo ni ya utalii.
Hivi sasa Rojo yupo Madrid, Hispania kwa ajili
ya kusubiri kuhojiwa na watumishi wa Ubalozi
wa Uingereza ambao watatathmini kwa kina
ugomvi aliosababisha wakati huo, na wakiona
inafaa watampatia visa ya kufanya kazi nchini
Uingereza. Fernando Burlando ambaye ni
mwanasheria wa Rojo, amedai kwamba
mchezaji
huyo aliyekuwa kwenye Timu ya Taifa ya
Argentina ameshaonekana na polisi kuwa na
kesi, hivyo anasubiriwa kupelekwa mahakamani,
lakini akasema watalimaliza suala hilo. Amedai
hata akitiwa hatiani, anaweza kuwekwa chini ya
uangalizi na kupewa adhabu ya kufanya kazi za
jamii, ambazo si lazima azifanyie nchini
Argentina, hivyo ataweza tu kuingia Uingereza.
Kabla ya mechi ya Jumamosi hii ya Man United
dhidi ya Burnley iliyoisha kwa suluhu, Van Gaal
alisema; “ni suala la muda tu. Mimi ni kocha
wa
klabu kubwa zaidi duniani lakini siwezi kubadili
sheria.” Baada ya mechi hiyo, akasema;
“naamini kwamba tutakapocheza na QPR
atakuwa ameshaipata (visa).”
Sunday, 31 August 2014
HAYA NDO MAPYA YALIYOBUKA OLD TRAFORD KUHUSU ROJO
Related Posts:
Tetesi zote za Usajili wa wachezaji barani Ulaya siku ya leo.Dau la Manchester United la pauni milioni 110 kwa Real Madrid kumtaka Gareth Bale, 25 na beki Rafael Varane, 22 limekataliwa na klabu hiyo ya La Liga (Daily Express), Real Madrid wana uhakika wa kumsajili kwa pauni m… Read More
Berbatov afungashiwa virago Monaco. MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa waBulgaria, Dimitar Berbatov anatafuta timu ya tatu ya kujiunganayo England, baada yakutemwa na AS Monacoya Ufaransa. Berbatov alijiunga na vigogo hao wa Ligue 1 Januari mwaka 2014 ku… Read More
Maneno ya Blatter baada ya kujiuzulu. “Nilijiskia mkamilifu kwa kugombea tena kwenye uchaguzi wa FIFA nikiamini kwamba kilikua ni kitu muhimu kwa FIFA. Uchaguzi umeisha lakini changamoto za FIFA hazijaisha. Japokua nina madaraka kutoka kutoka kwa wanachaman… Read More
BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika kurasa za magazeti yote ya leo Jumatano,June 03 MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhi… Read More
Uzinduzi wa jezi mpya Tifa Stars kuambata na tuzo maalumu. SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), kesho Jumatano linatarajia kuzindua jezi mpya za timu za Taifa Tanzania, zitakazokuwa zikitumika katika michuano mbalimbali, uzinduzi huo utakafanyika katika hoteli ya JB Belmonte (PS… Read More
0 comments:
Post a Comment