Facebook

Monday 25 August 2014

BALOTELLI AJIUNGA RASMI LIVERPOOL

Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli, 24,
amekamilisha uhamisho wake kutoka AC
Milan kwenda Liverpool kwa pauni milioni
16. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester
City, amekubali mkataba wa muda mrefu,
ingawa hatoweza kucheza dhidi ya timu yake
ya zamani Jumatatu usiku. Balotelli aliondoka
City miezi 17 iliyopita baada ya kupachika
mabao 30 katika misimu mitatu.
"Uhamisho huu unawakilisha misingi ya klabu
na nadhani tumefanya biashara nzuri tu
hapa," amesema bosi wa Liverpool, Brendan
Rodgers. Balotelli, ambaye atavaa jezi namba
45, amesema alifanya makosa kuondoka
England mwaka jana. "Nimefurahi kurejea
tena, kwa sababu nilifanya makosa kuondoka
England," amesema na kuongeza "Nilitaka
kwenda Italy, lakini nikagundua ni makosa."

0 comments:

Post a Comment