Facebook

Monday 25 August 2014

Mwanafunzi wa darasa la saba abakwa na "Muuza Genge"



Kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala,Jijini Dar es Salaam.
kuna faili la kesi namba MBL/RB/ 9817/2014- KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI ambalo linamsaka kijana Juma Athumani (30), mkazi wa Charambe, Mbagala kwa kosa la ubakaji wa mwnafunzi wa darasa la saba. 


Habari za kiintelijensia zilizotufikia BantuTz.com zilidai kwamba mtuhumiwa huyo ambaye ni muuza genge, alitenda kosa hilo Agosti, mwaka huu ambapo mwanafunzi huyo alikuwa ametumwa na mama yake gengeni.

Ilisemekana kwamba jamaa huyo alimuomba mwanafunzi huyo wazungumze kidogo ndipo akampeleka gesti kwa lazima.
 

Akizungumza na chamzo zhetu,mwanafunzi huyo alisema kuwa alipofika gesti, jamaa huyo alilipa fasta na kumvutia chumbani ambapo alianza kumshika sehemu za maziwa‘manido’ kisha akamtupia kitandani na kumwingilia kimwili bila ridhaa yake.

Alisema kwamba, jamaa alipomaliza shida zake, alimpa shilingi Elfu tano (5,000/=) lakini alipokataa huku akilia ndipo mwanaume huyo akamuongezea hadi ikafika buku kumi (10,000/=).
 

“Niliporudi nyumbani mama aliniuliza kwa nini nimechelewa kisha
akaziona hela, akaniuliza nimezipata wapi, nikamwambia amenipa Juma ndiyo tukaenda hadi gengeni kwa Juma kuuliza ndiyo mama akagundua kuwa nimebakwa.

“Baadaye mama alikwenda kuripoti polisi ndipo Juma akakamatwa na mimi nikapelekwa hospitali na kugundulika kweli nilikuwa nimebakwa,” alisema mwanafunzi huyo.


                Imeandaliwa na............
                                                      JAMES NICHOLAUS
                                                         {Admin BantuTz}

0 comments:

Post a Comment