Facebook

Monday 25 August 2014

Tetesi za Usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya na BantuTz SPORTS.

>Manchester United wamekamilisha
majadiliano na Real Madrid na watalipa pauni
milioni 63.9 na kuvunja rekodi ya Uingereza
kumnunua winga Angel Di Maria (Sky Sports),

>Mchezaji huyo kutoka Argentina huenda
akafikia kuuzwa kwa pauni milioni 72, milioni
60 zikilipwa mwanzo na milioni 12 baadaye
(Daily Mirror),

>Juventus wataanza
mazungumzo na Arsenal kuhusu Lukas
Podolski. Juventus wanamtaka kwa mkopo
lakini Arsenal wanataka kumuuza (Daily
Telegraph),

>Meneja wa Real Madrid Carlo
Ancelotti amesema Sami Khedira, 27,
hatoondoka licha ya kufuatiliwa na Arsenal,
Bayern Munich na Manchester United
(Guardian),

>Meneja wa Everton Roberto
Martinez amesema bado anaweza kumsajili
Samuel Eto'o, 33, au Danny Welbeck, 23,
katika wiki ya mwisho ya dirisha la usajili
(Times),

>Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amemuulizia kiungo mkabaji wa Brazil Luiz
Gustavo, 27, anayechezea Wolfsburg (Daily
Mirror),

>Southampton wamepanda dau kwa
winga wa Tottenham Andros Townsend, 23,
(ESPN FC),

>Meneja wa Southampton Ronald
Koeman yuko tayari kuanza kumfuatilia tena
winga wa Norwich Nathan Redmond, 20,
(Sun),

>Liverpool watalazimika kuchukua hatua
za haraka kumsajili Radamel Falcao, 28,
wakati Juventus wakimtaka mshambuliaji
huyo wa Monaco kwa mkopo (Daily Star),

>Fernando Torres hatoondoka Chelsea bila ya
mkataba wa kitita cha pauni milioni 8.5
kutolewa. Roma wanamtaka mshambuliaji
huyo (Sun),

>Sunderland wamekuwa na
mazungumzo na winga wa zamani wa Chelsea,
Salomon Kalou, 29, ambaye pia anatazamwa
na Arsenal, Liverpool na Everton (Daily
Express),

>Meneja wa Sunderland ana matumaini
ya kupata jibu iwapo mshambuliaji wa
Liverpool Fabio Borini, 23, atajiunga nao au
la (Sunderland Echo),

>West Ham
wamemuulizia beki wa Manchester City Micah
Richards, 26, ambaye anaonekana huenda
akaondoka City wiki hii (Sun),

>QPR wamehusishwa na kipa wa Reading Alex
McCarthy, 24, (Daily Star),

>AC Milan
wanamtaka Samuel Eto'o na Fernando Torres
kuziba pengo la Mario Balotelli (Gazetta dello
Sport),

>Juventus wana nafasi kubwa ya
kumshawishi Radamel Falcao kujiunga nao
kwa mkopo wa mwaka mmoja (Gazetta dello
Sport),

>Lukas Podolski huenda akasaini
mkataba wa miaka mitatu na Wolfsburg na
watalipa euro milioni 12 kumsajili kutoka
Arsenal (L'Equipe).

Zimesalia siku saba kabla
ya dirisha la usajili kufungwa kuwa karibu na BantuTz.com.

0 comments:

Post a Comment