Facebook

Monday, 25 August 2014

Carlo Ancelotti athibitisha kuhusu Di Maria kuaga wenzake.

IMG_6651.JPG
Sakata la usajili wa winga wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria kwenda klabu ya Manchester United limechukua sura mpya leo hii.
Kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kocha wa Real madrid Carlo Ancelotti amethibitisha mchezaji huyo yupo karibuni kuhama.
Di Maria jana hakufanya mazoezi na wenzake na badala yake alienda kuwaaga wachezaji pamoja na viongozi wengine wa Madrid.
“Alikuja leo{Jana} asubuhi, lakini hakufanya mazoezi. Uhamisho wake bado haujakamilika wote ila anakaribia kuhama kabisa.
“Tunamshukuru kwa kila alichoifanyia hii klabu na tunamtakia kila kheri huko anapokwenda, uhamisho haujakamilika rasmi, ila kila kitu tumeshakubaliana,”
Ancelotti alisema.


Ingawa Ancelotti hakuitaja timu anayoenda Di Maria lakini vyombo vya habari ulaya vinaripoti kwamba DI Maria atakuwa mchezaji mpya wa Man united kwa ada ya £64 million.

Related Posts:

  • Pogba-"Ndoto zangu ni kucheza na Messi" KIUNGO wa Juventus, Paul Pogba amekiri kuwa ana ndoto za kucheza sambamba na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka jijini… Read More
  • Chelsea yaikosa saini ya mfungaji bora wa Serie A,Mauro Icard. Timu ya Chelsea imepigwa mweleka katika mbio zake za kumsajili mchezaji Mauro Icardi baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba mpya wa miaka minne na Inter Milan ya Italy. Mauro miaka 22 alikuwa anahusishwa na kuhamia Chelsea… Read More
  • Essien asaini mkataba wa miaka 2 Panathinaikos Nyota wa timu ya taifa ya Ghana na klabu ya AC MilanMichael Essien amesajiliwa na kilabu ya Panathinaikos ya nchini Ugiriki kwa mkataba wa miaka miwili. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa ya Panathinaikos mchezaji huyo mwen… Read More
  • Liverpool watangaza kumsajili Milner. Klabu ya soka ya Liverpool imetangaza kumsajili kiungo James Milner kutoka Manchester City kwa uhamisho huru.Liverpool wamesema kuwa wamekubaliana masuala binafsi na Milner na atajiunga na timu hiyo mwezi wa saba tarehe moj… Read More
  • McClaren kocha mpya Newcastle. Steve McClaren anatarajiwa kuthibitishwa kuwa Meneja mpya wa Klabu ya Ligi Kuu England Newcastle Wiki ijayo. McClaren, mwenye Miaka 54, ni Meneja wa zamani wa England na pia aliwahi kuwa Meneja Msaidizi chini ya… Read More

0 comments:

Post a Comment