Pichani ni mafundi wakiendelea kumalizia ujenzi wa chumba hicho.
Sayansi
 ya Teknolojia ikiwa inaendelea kushika kasi siku hadi siku, chumba hiki
 maalum kilichojengwa juu ya safu za milima ya Alpine iliyopo Ufaransa 
kimepata kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotokea sehemu mbalimbali 
Duniani kutokana na staili ya aina yake walivyokitengeneza kwa kutumia  
vioo vilivyozunguka kichumba hicho kidogo  hivyo kumuwezesha mtalii 
kuona kama vile yupo juu ya Dunia.
Unaambiwa
 sio rahisi kwa mtu mwenye roho nyepesi kuweza kusimama kwenye kichumba 
hicho kidogo kutokana na kuwa kileleni mwa mlima Alpine takribani  
umbali wa  mita 3800 kutoka usawa wa bahari ambapo utengenezaji wake 
ulichukua takribani muda wa miaka miwili na ada ya kutembelea kwenye 
kivutio hicho ni kiasi cha Euro 55 ambazo ni sawa na Tsh 80,000 bila 
chenji.
0 comments:
Post a Comment